Tanzania iendelee kuiunga mkono sahara magharibi
![]() |
| Mfalme mohamed wa VI wa Morocco |
Na: Rayusa Yasini Dar es salaam
mwambawahabari
KATIKA KUUNGA mkono msimamo wa Tanzania kuendelea kutambua sahara ya Magharibi kwenye vyombo vya Kimataifa ikiwemo umoja wa mataifa kamati ya Mshikamano wa Tanzania na Sahara Magharibi imeiomba serikali kuendelea na msimamo wake wa kui unga mkono sahara magharibi.
Mwito huo umetolewa leo DAR ES SALAM na mratibu wa haki za binadamu Alphonce Lusako alipokuwa anazungumzia ujio wa mfalme wa sita nchini , kuwa kisingizio cha kuizika misingi ya Tanzania ya utu’ udugu’ wa kuwapigania wanyonge waliogungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa katika magereza tofauti nchini humo.
Amesema jitihada za umoja wa afrika za kutambua na kupigania sahara magharibi kuwa huru pamoja na kutanua mamlaka ya minurso ili iweze kutizama masuala ya haki za binadamu,
‘’SISI ndugu zenu kutoka tanzania tutaendelea kuwaunga mkono kama alivofanya baba wa taifa mwalimu Julius kambarage nyerere pamoja na viongozi waliofuatia na wala hatutakubali kuuza utu na fahari yetu ya uhuru kwa sababu ya ushawishi wowote.
Kwa upande wake mratibu wa mawasiliano Noel Shao (TASSC) ameiomba serikali ya Tanzania kutoyumba katika msimamo wake kuhusu suala la sahara magharibi.
Mfalme wa sita toka Moroko anatarajia kufika nchini kesho kwa ziara ya siku tatu huku mwenyeji wake akitarajiwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania JOHN POMBE Magufuli na atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na sekta ya uwekezaji hapa nchini.

Post a Comment