Ads

SERIKALI YAANZA UTAFITI WA UPATIKANAJI NISHATI VIJIJINI

Na:John Luhende
Mwambawahabari
Asilimia 41 ya wakazi  wa vijijini nchini wamefikiwa na Huduma ya Umeme  inyosambazwa na   Wakalawanishati  vijijini REA ukilinganisha na asilimia  2% ya watanzania  waliokuwa wanapata Huduma hiyo mwaka 2007 kabla ya kuanzishwa kwa wakala huo.

Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi  mkuu wa wakala wanishati vijijini  REA Injinia   Gissima  Nyamuhanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari ,na kuongeza kuwa mafanikio hayo yamekuja baada ya serikali kutoafedha za kutosha kwaajili ya kugharamia miradi hiyo ambapo zaidi ya bilioni 587.7,nahalmashauri mpya  zote nchini zimeunganisha na Umeme.

Naye mkurugenzi wa Takwimu ya sensa ya watu na makazi  Dr Ephraim Kwesigabo amesema Sambamba na ukusunyaji wa takwimu hizo, Dkt Kwesibago alisema kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu za kidemografia na za kiuchumi za wanakaya zikijumuisha umri, jinsia, hali za ndoa, elimu, shughuli za kiuchumi, matumizi ya muda pamoja na ushiriki wa jinsia katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aliongeza kuwa utafiti huo utahusisha jumla ya maeneo 676 ya vijiji na mijini yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote ya Tanzania bara na kuhusisha jumla ya kaya binafsi 10,140 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopatikana katika maeneo yao.

Aidha, alisema kuwa timu ya wadadisi wapatao 130 watahusika katika zoezi hilo la ukusanyaji taarifa ambapo kila mkoa utakuwa na wadadisi watano, msimamizi mmoja na wataalamu wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu makao makuu.

Vile vile alisema kuwa upatikanaji wa takwimu hizo utasaidia katika kuandaa taarifa kuhusu hali halisi ya upatikanaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini na hivyo kuweza kupima na kuhakiki maendeleo yaliyofanikiwa na mafanikio ya juhudi za Serikali.

Pia  taarifa za utafiti huo zitatumika katika kuendeleza mipango ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali itakayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini.

Amesema utafiti huu ni  wa kwanza  kufanyika kwa kuhusisha mkoa yote bara ,kabla ya utafiti huu mwaka 2011 ulifanyika utafiti wa awali wa kutathimini  hali ya  upatikanaji wa Nishati  nchini ambao ulihusisha baadhitu ya mkoa  ya Tanzania bara, na amewataka wananchi  kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwa dhuru watafiti watakapo fika katika nakazi yao.

Sanjari  na ukusunyaji wa takwimu hizo, Dkt Kwesibago alisema kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu za kidemografia na za kiuchumi za wanakaya zikijumuisha umri, jinsia, hali za ndoa, elimu, shughuli za kiuchumi, matumizi ya muda pamoja na ushiriki wa jinsia katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aliongeza kuwa utafiti huo utahusisha jumla ya maeneo 676 ya vijiji na mijini yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote ya Tanzania bara na kuhusisha jumla ya kaya binafsi 10,140 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopatikana katika maeneo yao.

Vile vile alisema kuwa upatikanaji wa takwimu hizo utasaidia katika kuandaa taarifa kuhusu hali halisi ya upatikanaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini na hivyo kuweza kupima na kuhakiki maendeleo yaliyofanikiwa na mafanikio ya juhudi za Serikali.

Pia  taarifa za utafiti huo zitatumika katika kuendeleza mipango ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali itakayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini.

Mbali na hayo wananchi wameombwa kutochukua sheria mkononi kwa kuwadhuru watafiti wanapokuwa wakifanya tafiti mbalimbali  katika  maeneo yao kwa ajili ya kusaidia nchi kupata takwimu rasmi zinazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo.

No comments