Ads

RC MAKONDA:TANZANIA ITANUFAIKA NA ZIARA YA MFALME WA MOROCCO,AWATAKA WANA DAR ES SALAAM,KUCHANGAMKIA FURSA.

Mwambawahabari

Mfalme wa Moroco Mohammed VI  akiambatana na msafara wa watu wapatao 1000  anatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 23 mwaka huu katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mbali na ujio huo kwa mara ya kwanza nchi ya itaweka historia ya kuwasili ndege sita kubwa aina ya Boing  na ndege ndogo mbili kwa ajili ya shughuli za utalii, na kuhitimisha ziara hiyo Octoba 27.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda amesema Rais John Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wawekezaji wanakuja nchini kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi na kuitangaza kimataifa zaidi ambapo amesema ujio wa wageni huo utasaidia kwa kiasi kikubwa nchi kuingiza mapato katika suala zima la utalii na uchiumi.

PAMOJA na mambo mengine Mfalme Mohamed VI anatarajiwa kusaini mikataba ya kimakubaliano 11 akiwa na Mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli yenye tija kwa Taifa ikiwemo katika masuala ya kilimo kwa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo pembejeo za kilimo, masuala ya mifugo na uvuvi, nishati na madini, masuala ya utalii ambapo kuna ndege mbili za ugeni huo zitatumika kwa ajili ya utalii pekee, pia ujio huo utadumisha ushirikiano wa kisiasa na kushirikiana kwa Wizara za Mambo ya nje za Moroco na Tanzania.


No comments