Ads

Rais Magufuli aongoza mamia Ya Wananchi kumuaga Dk Masaburi

Mwambawahabari


Rais John Magufuli leo ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuuga mwili wa aliyekuwa meya wa jiji hilo, Dk Didas Masaburi aliyefariki Jumatano iliyopita na kusema Masaburi ana wake wanne au watano na watoto zaidi ya 20.

Kauli ya Dk Magufuli ameitoa muda mfupi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk Masaburi kusema kuwa ameacha mke mmoja waliyefunga naye ndoa Jannet Masaburi na wajane wawili kauli ambayo ilizua miguno kutoka kwa waombolezaji.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza Dk Magufuli alisema anamfahamu Dk Masaburi kuwa alikuwa  na wake wanne au watano hivi.

Alisema hata watoto anafahamu kuwa anao zaidi ya 20.Rais Magufuli alisema Masaburi alikuwa rafiki yake,ndugu yake na mpiganaji mwenzake ndani ya CCM.

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kichama wakiongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli (wa tano kulia) wakiwa katika viwanja vya Karimjee mapema leo asubuhi kutoa heshima ya mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Dkt Didas Masaburi,aliyefariki wiki iliopita katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili,wakishiriki 
Baadhi ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili wa mpendwa wao Dkt Didas Masaburi 

No comments