Ads

OMEGA MINISTRY CHURCH OF ALL NATIONS YAANDAA SEMINA YAKUOMBEA TAIFA




Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa.



Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry.


 Waandishi wa habari ya wakifuatili jambo wakati wa mkutano wao na Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry leo Jijini Dar es Salaam.

Picha na Frank Shiuja,

Mwambawahabari
Lilian Lundo, 
KANISA la Omega Ministry of All Nations lenye makao yake Makuu Mbezi Afrikana, Jijini Dar es Salaam limeandaa Semina ya Injili ya Neno la Mungu la kuiombea Taifa na Viongozi wa Nchi, inayotarajiwa kufanyika Urafiki Nyangumi Jijini Dar es Salam Octoba 21 mpaka 23 mwaka huu.

Nabii Samson Rolinga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Semina hiyo yenye lengo la kuiombea Taifa, Viongozi wa Nchi na kuwafungua watu katika vifungo mbalimbali.
“TutaliombeaTaifa lirudi katika misingi ya Mungu, vile vile tutawaombea watu waliofungwa na nguvu za giza na magonjwa kama vile kanda, ukimwi na utasa,” alifafanua Nabii Rolinga.

Amesema magonjwa yapo lakini pia yapo magonjwa ambayo yanatengenezwa na watu ilikumdhoofisha mtu, hivyo katika semina hiyo kutafanyika maombi ya kuombea magonjwa hayo pamoja na matatizo yote yanayotokonana roho za kurithi.

Vile vile amesema kuwa kumekuwa na matatizo mengi sana ambayo watu hawana majibu ya matatizo hayo mfano vijana wengi kutokuwa na kazi na kukata tama huku wakijraribu kupambana na matatizo hayo kwa njia ya mwili.

Nabii Rolinga amesema kuwa lengo lake nikuonyesha chanzo cha matatizo na kuyatatua kwa njia ya maombi pamoja na kueleza namna ufalme wa giza unavyofanya kazi.

Kwa upande wake Nabii Donald kutoka Mwanza amesema kuwa atakuwepo katika semina hiyo ambayo itashughulikia matatizo ya Roho, kuvunja yanayoonekana katika ulimwengu wa Roho pamoja na kuombea nchi na Utawala wa nchi.

Aidha amesema kuwa watumishi wa Mungu wana jukumu kubwa la kuwaombea Viongozi wa Nchi na Rais ili Mungu awasimamie katika majukumu yao ya kila siku ya kuliongozaTaifa.

No comments