MAGEMBE AKEMEA CHUO CHA UTALII KWA UCHAFU
Na Maria Kaira
Mwambawahabari
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ameutaka uongozi wa chuo cha taifa cha utalii kutoa elimu inayoendana na mahitaji ya sekta hiyo ili kuweza kuibua wahitimu wenye vigezo na taaluma hiyo kwa lengo la kulilitea taifa maendelea.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam alipotembelea katika chuo hicho na kukuta baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kuutaka uongozi kuyabadirisha mapungufu hayo ili chuo hicho kiwe cha mfano.
Prof. Maghembe amewataka wakufunzi wa chuo hicho kuboresha mafunzo wanayotoa kwa wanafunzi wao hususani ya vitendo na lugha yawe yanakidhi vigezo kwa kuwa utalii ni kitu muhimu katika taifa ikiwa sekta hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato la nchi.
Pia Maghembe amesema Chuo kinatakiwa kujikita kuwafundisha wataalamu wa taaluma hiyo kozi ya ukarimu ili kuwasaidia katika kazi zao watakazozifanya ili waweze kupata kipato.
" katika sekta ya utalii ukarimu ni kitu muhimu sana kinachotakiwa wanafunzi wetu wazingatie sana Sio mgeni anafika hamuoneshi ukarimu wanaanza kumshangaa tu unafikiri ataweza kurudi tena siku nyingine, pia wanatakiwa wajue vizuri kuongea lugha za kigeni ili waweze kumvutia mgeni kuja kwa Mara nyingine" amesema
Aliongeza kuwa ni lazima chuo kiweze kutumia njia ya kuwapima wanafunzi hao kabla ya kuhitimu na kuweza kujua walichofundishwa darasani wamekizingatia katika kutoa huduma iliyobora na safi kwa wageni na sio bora huduma.
" Muendeshe chuo kwa kuangalia miongozo na kuangalia utaratibu wa chuo unavyoendelea sio mtu amehitimu ukimpeleka katika hotel ya nyota tano haelewi vitu vinavyoitajika au hana ukarimu hiyo inakuwa haipendezi katika sekta hii" amesema
Hata hivyo profesa Maghembe amewasisitiza watu wa sekta ya utalii kupenda Usafi ili kuwa kivutio kwa wageni na kupitia sekta hiyo.
" Nimesikitishwa kukuta hali ya uchafu katika chuo hiki, ikiwa chuo hiki ndio kinahusika na mambo ya utalii "

Post a Comment