Ads

JINA LA RC MAKONDA LATUMIKA NA MATAPELI KUPIGADILI DAR, KAMISHINA SIRRO ATOA ONYO KALI


Mwambawahabari
Kamanda wa Polisi  Kanda Mwalimu ya Dar es salaam Kamishina  Simon Nyakoro Sirro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika ukumbi wa polisi kituo cha kati jijini Dar es salaam (picha na John Luhende)


Na Maria Kaira,Dar 
Mwambawahabari
Polisi Kanda Maalum Dar es salaam lina watahadharisha wakazi  wa Jiji la Dar es salaam na wageni kutoka mikoani pamoja na raia wa kigeni kuwa makini na wahalifu wanaotumia majina ya viongozi wa serikali ili kujipatia fedha kinyume na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa polisi kanda Maalum Dar es salaam  Saimon Sirro amesema kuna malalamiko mbalimbali yamejitokeza kwa raia wa kigeni kwamba kunabaadhi ya wahalifu wanatumia vibaya jina la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na kujihusisha kuomba fedha za kimarekani na za Tanzania kwa madai ya  kuwasaidia wanafunzi kupata vyuo nchi za nje.

Amesema tukio la kwanza lilitokea Octoba 1 raia wa China Marco Li (24) mfanyabiashara wa kampuni ya Group Six International mkazi wa mikocheni B aliweza kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu na kujitambulisha jina la mkuu wa mkoa Paul Makonda akimtaka atoe dola 3500 za kimarekani kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi aliyechaguliwa chuo kikuu cha Manilla kilichopo nchini Ufilipino.


"Mkurugenzi wa kampuni ya Group Six International Jensen Hung alikubali ombi  hilo na kuchangia fedha sh.7,595,000 akiamini simu aliyopigiwa na kuombwa msaada ni ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kumbe ni matapeli, wakazi wote wanapaswa kuwa makini na matapeli hao" amesema

Kamishna Sirro amesema Octobar 28 saa mbili na robo usiku maeneo ya Vigozi Mbagala jeshi hilo waliweza kupambana na majambazi watatu wakiwa na silaha aina ya SMG waliotaka kupora katika maeneo hayo,ambapo polisi walifanikiwa kuichukua silaha hiyo iliyofutwa namba huku majambazi hao walikimbia kusiko julikana juhudi za kuwatafuta zinaendelea.

Aidha jeshi hilo limefanikiwa kukamata panya road watatu waliovamia nyumba ya Ladislaus Kaitaba (58) ambaye ni askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania.

" katika ufatiliaji wa tukio hilo tumemkamata Ramadhani Ndabi (35) mkazi wa Mbagala Charambe akiwa na simu iliyoibiwa eneo la tukio baada ya kufanyiwa upekuzi katika chumba anachoishi tulimkuta na mapanga saba mapya ambayo alieleza ndio anayoyatumia kufanyia uhalifu" amesema

Hata hivyo katika mahojiano waliyofanya aliweza kuwataja washiriki wenzake huku ukamataji ukiendelea, waliokamata ni pamoja na Saidi Matimbwa (25) mkazi wa charambe na Hamadi Iddi, pia opareshine hiyo inaendelea ili kuweza kuwakamata watuhumiwa wote walioweza kuhusika katika tukio hilo.

No comments