JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DSM LAONYA KUHU UTAPEL JIJINI
Mwambawahabari
Na Maria Kaira Dar
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewatahadharisha wananchi wa jiji la Dar es salaam kuwa makini na matapeli wanaotumia njia ya kuwarubuni watu kwa kuwatafutia ajira huku wakiwa na lengo la kuwatapeli Fedha zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro amesema watu hao wanajifanya wanawatafutia watu ajira kwa mashariti ya mteja kwa kulipia baadhi ya garama kwa ajili ya jopo la watu watakaofanyiwa usaili.
Kamanda Sirro amesema makampuni hayo yamekuwa yakitoa masharti rahisi ili kuwapata wateja wengi na kukusanya Fedha nyingi zisizo za halali.
" nawatahadharisha wakazi wa jiji la Dar es salaam kuwapuuza matapeli hao na watupe ushirikiano kwa kutoa taarifa hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao" amesema.
Pia amesema jeshi hilo linatoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao wanajitokeza kutoa taarifa za uongo za uhalifu unafanyika katika eneo fulani lakini polisi wakifika sehemu ya tukio hawakuti ualifu wowote .
"ufuatiliaji kupitia mitandao ya simu unaendelea ili kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria pia wananchi waendelee kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa za kweli "amesema
Aidha amesema wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 87 kwa nyakati tofauti tofauti maeneo mbalimbali wakiwa na makosa mbalimbali,baadhi ya watuhumiwa hao walipatikana wakiwa na gongo lita 148 ,bhangi kete 95 na puli 48 ambapo watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Wakati huo huo kamanda Sirro amesema kanda maalum Dar es salaam kupitia kikosi cha usalama barabarani limefanikiwa kukusanya sh 541,830,000 kupitia tozo mbalimbali za makosa ya usalama wa barabarani.
Post a Comment