Ads

HATUNA MPANGO WA UANZISHWAJI VISA YA PAMOJA YA UTALII :WIZARA YA MAMBO YANJE





Na Maria Kaira 
Mwambawahabari
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki imesema hakuna mfumo wowote wa uanzishwaji wa visa ya pamoja ya Utalii kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanzishwa na badala yake bado wapo katika majadiliano baina yao.

Ufafanuzi huo umetolea na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Uwekezaji Sekta ya Uzalishaji Bernard Haule na kuutaka umma wa watanzania kuelewa  kuwa majadiliano ya Nchi wanachama kupitia vikao vya sekta ya utalii na wanyamapori  upo katika majadiliano katika  Nchi Wanachama ili kuweza kufanikisha azma hiyo.

Pia utafiti uliofanyika mwaka 2010, ulibainisha kujenga uwezo wa watumishi kwenye suala la mfumo wa kieletroniki wa utoaji viza ya pamoja ya utalii, kuwepo kwa maafisa uhamiaji katika kila ofisi za ubalozi.
Haule amesema serikali inapenda kuwahakikishia umma wa Tanzania kuwa itaendelea kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya Jumuiya na kushiriki katika majadiliano ya kuanzisha visa ya pamoja ya utalii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

" Hakuna viza yoyote ya pamoja ya utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokubalika taarifa zilizotolewa na kuripotiwa hazina ukweli wowote zilikuwa na lengo la kuichafua serikali ' amesema.

Aliongeza kuwa mkutano wa tano wa baraza la kisekta la mawaziri wa utalii na usimamizi wa wanyamapori uliofanyika julai 2013 jijini Bujumbura uliweza kuagiza kuundwa kwa kikosi kazi Ili kuandaa mpango kazi na uanzishwaji wa viza ya pamoja ya utalii.

" chakushangaza kabla ya utekelezaji wa maagizo hayo kutekelezeka nchi ya Uganda, Kenya na Rwanda walianzisha viza ya pamoja ya utalii baina yao nje ya vikao vya Jumuiya.

No comments