WATALAAM WA TEHAMA TUMIEN TEKNOLOJIA MPYA;PROF KAMUZOLA
Mwambawahabari
Na Ally Daud
Wataalamu Wa tehama wamepaswa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ya tehama ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo iliyopo kwa sasa ulimwenguni.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustin Kamuzora katika mkutano wa wadau wa tehama uliojadili utekelezaji wa mkakati wa Sera ya Tehama ya mwaka 2016
Aliongeza kuwa wataalamu wa tehama wanapaswa kutumia njia mpya na za kisasa ili kukuza uchumi kama zinavyofanya nchi zilizoendelea duniani.
"Wanatehama mnatakiwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ili kuweza kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati kwa kupitia teknolojia hiyo kama zifanyavyo nchi nyingine zilizoendelea duniani kote" alisema Prof. Kamuzora.
Aidha Prof. Kamuzora alisema katika mkutano huo wanatarajia kupata mbinu mbadala za kupambana na uhalifu kwa kutumia mitandao katika kutekeleza mkakati wa Sera ya tehama ya mwaka 2016- 2020 ili kutekeleza mpango huo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza alisema kuwa moja ya mkakati wa mkutano huo ni kutengeneza miundombinu ya tehama kwa Watanzania waweze kufikiwa kirahisi.
Aidha mhandisi Ichwekeleza alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2018 inaandaa mkakati maalum wa kuwalinda watoto kutokana na madhara ya Tehama ili kuweza kuwasaidia watoto kukua katika misingi bora inayoendana na jamii ya Tanzania.
Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali Wa mitandao ya simu pamoja na wataalamu Wa tehama nchini ili kujadili mkakati wa Sera ya Tehama ya mwaka 2016.

Post a Comment