WAMACHINGA KARIKOO WAIKOSESHA MAPATO, TRA.
| Meneja madeni na ushurutisha wa TRA mkoa wa Kodi Ilala Nuhu Msangi mwenye koti jeusi kulia akimsikiliza kwa makini mtendaji wa mtaa wa kariakoo hayupo pichani (picha na John Luhende) |
Na: John Luhende
mwambawahabari
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Leo imeendesha mafunzo maalumu kwa watendeji wa Mataa na Kata katika wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, yenye lengo la kujenga mahusiano bora na watumishi hao ili kuongeza makusanyo ya kodi katika wilayahiyo.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Leo imeendesha mafunzo maalumu kwa watendeji wa Mataa na Kata katika wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, yenye lengo la kujenga mahusiano bora na watumishi hao ili kuongeza makusanyo ya kodi katika wilayahiyo.
Akizungumza katika mafunzo hayo , Afisa Elimu na Huduma wa mkoa wa kodi Ilala bwn Zakeo Kowero amewataka watendaji hao kusaidia malakahiyo kwa kuwahamasisha wananchi kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kulipa kodi kwa uaminifu.
Wakichangia mada katika mafunzo hayo baadhi ya watendeji hao wamesema suala la wamachinga kuruhusiwa kufanya biashara katikati ya jiji limeathiri kwa kiasi kikubwa makusanyo ya mapato katika mkoa huo,na kuongeza kuwa wengi wa wafanyabiashara hao siyo wamachinga kila niwafanya biashara wakubwa na vigogo wamejificha nyumao na wametaka kuandaliwa utaratibu mpya badala ya huo.
![]() |
| Baadhi ya watendaji wa mkoa wa kodi Ilala wakifuatilia mafunzo yaliyo endeshwa na mamlaka ya mapato hawapo pichani (picha na John Luhende). |
Naye Meneja msaidizi madeni na ushurutishaji , Nuhu Msangi amesema suala la wamachinga kufanya biashara kariakoo nisuala mtambuka lina takiwa kutazamwa kwa umakini kwa kuwa linagusa mamlaka nyingi ikiwemo Serikali kuu.


Post a Comment