TIC YASAJILI MIRADI YA UWEKEZAJI 198 MKOANI MOROGORO.
Mwambawahabari
Na.John Luhende
Kituo cha uwekezaji kimesema hatua ya serikali kuhamishia makao makuu yake mkoani Dodoma kumefungua fursa nyingi za uwekezaji katika mikoa jirani hasa mkoani Morogoro ambao una eneo kubwa linalo faa kwa uwekezaji wa kilimo, na viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa kituo hicho Clifford Tandari amesema kituo cha uwekezaji nchini kwa kushirikiana na mkoa wa Morogoro wame andaa mkutano Mkubwa wa kuhamasisha na kukuza uwekezaji na biashara mkoani huko mwishoni mwa mwezi huu.
Amesema,Kituo hicho mpaka Sasa kimweweza kusaji miradi 198 ambapo vote itaelekezwa mkoani Morogoro na inatarajiwa kuzalisha ajira ziapatazo 28,944 ambapo ambapo katika miradi 111 ni ya watanzania ,miradi 41 ni ya wageni na miradi 46 ni ya ubia kati ya wageni na watanzania .
Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe amesema mkoa huo umejaaliwa kuwa na fursa na mazingira mazuri ya uwekezaji,na lasili Mali nyingi ambazo bado hazija tumika ipasavyo na wakati umefika Sasa kwa wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo.
Post a Comment