TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YAH: JINA SAHIHI LA AKAUNTI YA KUCHANGIA MAAFA KAGERA
Mwambawahabari
Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu Maafa inaendelea kuwapa wananchi pole na janga la tetemeko lililotupata katika mkoa wa kagera tarehe 10.09.2016.
Aidha Kitengo cha Maafa kinapenda kutaarifu umma kwamba jina sahihi la akaunti ya Maafa ni KAMATI MAAFA na sio KAMATI YA MAAFA.
Pia Idara inasisitiza watu mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kupitia akaunti Rasmi zifuatazo:
CRDB BANK BUKOBA
Akaunti Na: 0152225617300
Swiftcode: CORUtztz
M-pesa: 0768196669
Tigo Pesa: 0718069616
Airtel Money: 0682950009
Idara inakaribisha taarifa za maoni, malalamiko au jambo lolote kutoka kwa waathirika wa
tetemeko la ardhi kupitia kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera kwa simu namba zifuatazo:
OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA-Simu namba 0621155777
KITENGO CHA MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU: 0621155888
IMETOLEWA NA:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Waziri Mkuu
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
SEPTEMBA 20, 2016
kamati maafa ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa

Post a Comment