MUHIMBILI KUTUMIA MILIONI 528 KUSOMESHA WATAALAMU WAKE NJE
| Kaimu mkurugenzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili Pro.Lawrence Museru , akizungumza na waandishi wa habari Muhimbili Leo ( picha na John Luhende) |
Na .John Luhende
Mwambawahabari
Hospital ya Taifa ya Muhimbili imesema katika kutimiza azma ya serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje yanchi kutibiwa ,septemba 25 mwakahuu itapeleka wataalam saba nchini India katika hospital ya Apollo Newdel ili kujifunza kwa vitendo kufanya upasuaji nakupandikiza kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto.
Hospital ya Taifa ya Muhimbili imesema katika kutimiza azma ya serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje yanchi kutibiwa ,septemba 25 mwakahuu itapeleka wataalam saba nchini India katika hospital ya Apollo Newdel ili kujifunza kwa vitendo kufanya upasuaji nakupandikiza kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi wa hospital hiyo Prof Lawrence Museru amesema wataalamu hao watakaokwenda ni pamoja na madaktari bingwa wawili wa upasuaji wa pua, koo namaikio ,wauguzi wawili wa chumba cha upasuaji,mtaalamu mmoja wa kupima usikivu pamoja na wataalamu wawili wakufundisha jinsi ya kuongea kwa watoto Salio zaliwa na matatizo hayo.
Aidha prof Museru amesema wataalamu hao wanatarajiwa kurejea okctoba 28 mwaka huu tayari kwa kuendelea kutoka Huduma hiyo na safari yao itagharimu shilingi milioni 528 zikijumuishwa na gharama za mafunzo,nauli ,gharama za kujikimu na za mafunzo mengine na Hospital hiyo itagharamia hudua hizo.
Amesema kuwa Hospital hiyo inatarajia kutumia kiasi cha shilingi billion 3.4 kwaajili ya kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 12 hadi 20 ambapo Sasa wanafanya ukarabati wa Vyumba 12 vilivyopo na kuweka vifaa vipya katika Vyumba vya upasuaji vitakavyo ongeza eneo la Huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo na kuongeza Vitanda kutoka 17 vya Sasa hadi 42 pamoja na kuongeza machine kufikia 42 na kuwaeka mtambo wa kuchuja maji.
Museru ameeleza kuwa Hospitali pia itaongeza vyumba vipya vinne vya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalum (ICUs) vikiwa na Vitanda 40,vifaa maalumu na vyumba 4 vya kupokea wagonjwa baada ya kutoka ICU (step- down ICU) vitanda 40 na ukarabati wa miundombinu uta kamilika mwishoni mwa mwakahuu.
Akijibuswali alilo ulizwa na waandishi kuhusu kutumia fedhanyingi kupeleka wataalamu nje kusoma badala ya kuleta waalimu wakawafundisha hapa hapa nchini prof Museru alisema
''Tanzania haiwezi kuwa Kisiwa hasa kwa utaalam kama huu unaotuona hapa wote tulijifunza kwa wenzetu na kupata uzoefu , wana waeza kufunzwa hapa lakini waka kosa uzoefu, unapokuwa huko unajifunza mengi hata nje ya masomo ila hata utendaji Kazi kwa vitendo" aliongeza prof Museru
Post a Comment