Ads

LHRC YA ADHIMISHA MIAKA 21 NA WATOTO YATIMA KURASINI, YAITAKA SERIKALI KUFANYIA MAREKEBISHO SHERIA YA WA TOTO.

 Mwambawahabari
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC ) bi,Hellen Kijo Bisimba akikabidhi misaada kwa mwkilishi wa watoto wa makao ya watoto kwenye shida Kurasini Temeke Jijini Dar es salaam,ambapo kitihicho kilijumuika na watoto hao katika kuadhimisha miaka 21 tangu  kuanzishwa mwaka 1995.(picha zote na John Luhende)

Na, John Luhende.
Mwambawahabari
Kituo cha sheria na haki za binadamu  kimeiomba serikali kupitia wizara ya Afya ,Jamii jinsia ,wazee na watoto, pamoja na na wizara ya katika na sheria ,kufanya marekebisho ya sheria ya mtoto  nakutilia mkazo malezi bora ya watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakacho toa  adhabu kali  kwa familia itakayo shindwa kutoka malezibora kwa watoto.



Badhi ya wafanya Kazi wa LHRC wakiwa wamejumuika na watoto wa kituo kulea watoto wenyeshida,aliyeko upande wa kulia ni Mwanasheria  Lulu  Urio.
Akizungumza katika maadhimisho ya  miaka 21 ya kituo cha sheria na haki za binadamu, yalifanyika katika kituo cha watoto wenye shida kurasini Temeke Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi mtendaji wa  kituo hicho bi, Hellen Kijo Bisimba,  amesema kuboreshwa kwa sheria hizo kutasaidia kupunguza wimbi la watoto wasio na makao maalumu  wanao zagaa kuomba omba mitaani, na ameitaka jamii  kushiriki katika kutatua tatizo la watoto wa mitaani linalozidi kushika Kasi kila siku.

Maafisa wa LHRC  wakifurahi  na kuimba pamoja na watoto katika madhimisho ya miaka 21 ya Kituocha sheria na haki za bina  damu.

 Aidha Bisimba  amesema ,sababu za kuwepo kwa watoto wa  mitaani   kumechangiwa na ndoa na mimba za utotoni , wanawake kutelekezwa na waume zao hali ambayo huchangia kuwazaa watoto na kuwatupa ,mahusiano mabaya baina ya wazazi ,ukatili wanao fanyiwa watoto na familia zao, familia kusambaratika ,malezi ya mzazimmoja ,malezi ya Bibi,shangazi, walezi wengine  , ulevi uliopindukia ,mfumo dume ,mila na desturi zilizo pitwa na wakati halingumu ya uchumi  na umasikini ulio kithiri.



Afisa mfawidhi wa makao ya Taifa ya watoto kwenye shida kilichopo kurasini, Beatrice Laurence   akizungumza na wgeni waliofika kutembelea makao hayo 

Amesema, hali ya ukatili kwa watoto nchini kulingana na ripoti za  Jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia  kwa mwaka  January hadi machi  2016 inaonyesha kuwa matukio ya  kubakwa na kulawitiwa watoto yanazidi kuongezeka kutoka 180 hadi 1765 ,kulinganisha na matukio 1585 yaliyo ripotiwa mwaka 2015 ,ambapo watoto wa kike na  kiume walio lawitiwa  na kubakwa katika kipindi cha miezi saba  walikuwa 2571, na miongoni mwa kesi  hizo  1203  bado zipo katika hatua ya upelelezi  na kesi 822 ziko mahakamani na watuhumiwa 234 wamekwisha hukumiwa.




Naye afisa mfawidhi wa kituo  hicho  Beatrice Laurence  ame kishukuru kituo cha sheria na haki za Nina damu kwakuona umuhimu wa kutoka misaada katika kuwa saidia watoto wanao lelewa  hapo  nakuwataka watanzania wengine  badala ya kuelekeza nguvu zao  pekee kwa wathirika wa tetemeko huko Kagera  kuwa kumbuka na  watoto yatima kwani nao  wanayo kahitaji ya kibinadamu.


Badhi ya vitu vilivyo tolewa msaada na LHRC katika makao ya watoto wenyeshida(picha zote na John Luhende). 


No comments