Waziri Mkuu awataka Mawazi kuzingatia Maadili
Na Anitha Jonas
mwambawahabariblog
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim
Majaliwa amewaasa Mawaziri na Manaibu Waziri kuzingatia sheria ya Maadili kwa
Viongozi wa Utumishi wa Umma kwani maadili ni nyenzo kubwa katika
kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Mheshimi wa Majaliwa ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es
Salaam alipokuwa akifungua semina ya Maadili kwa Mawaziri na Manaibu Waziri
inayolenga kuwajengea uwezo mkubwa yanamna kiongozi wa utumishi wa umma anavyotakiwa
kutekeleza majukumu yake bila kukiuka maadili.
“Chimbuko la Maadili ya Utumishi wa Umma ulianza tangu siku
nyingi na umekuwa ukitajwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo katika Katiba ya
nchi ya mwaka 1977, Sheria za Utumishi wa Umma pamoja na Kanuni za Utumishiwa
Umma,”alisemaMajaliwa.
Akiendelea kuzungumza katika Semina hiyo WaziriMkuu alisisitiza
kuwa Semina hiyo siyo semina elekezi kwa viongozi hao kama jinsi imekuwa
ikijadiliwa katika mitandao ya kijamii, bali ni semina inayolenga kutoa mwongozo
wa maadili ya viongozi wa umma na utekelezaji wa Hati ya Ahadi ya Uadilifu na
mada katika semina hiyo zitahusu masuala ya maadili tuu.
Kwa upande wa Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda
kutoka Ofisi ya Rais Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma
amesema semina ya maaadili kwa viongozi ni jukumu la Sekretariati ya maadili
kuandaa kwani hiyo ni sehemu ya majukumu ya Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Utumishi wa Umma na wao ndiyo wenye wajibu wakuhakikisha viongozi
wa utumishi wa umma wanazingatia maadili.
“Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma
inamamlaka ya kufanya uchunguzi kwa kiongozi yoyote wa umma atakayesikika
kukiuka maadili kama kiapo cha ahadi za uadilifu kinavyosema,”alisema Jaji Mstaafu
Salome.
Aidha Kamishna wa Maadili huyo aliendelea kusema Ofisi ya
Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya rasimali fedha ambapo wanazaidi ya miaka
mitatu wameshindwa kufanya uhakiki wa mali za viongozi pamoja na uchunguzi
kutokana na changamoto hiyo.
Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili
ya viongozi wa Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na
Shirika la USAID.
Post a Comment