WAZIRI ANGELA KAIRUKI ATUMBUA MAJIPU ,ALIYETUMBULIWA JIPU NUSURA AZIMIE MBELE YA WAZIRI
mwambawahabariblog (picha na mtandao)
WAZIRI wa nchi,ofisi ya Rais
menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora, Mh Angella Kairuki
amemsimisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro kutoka
na uzembe uliipelekea hasara serikali ya bilioni 1.
Vilevile Waziri Kairuki
amewasimamisha pia mkuu wa chuo hicho tawi la Dar es
salaam,Joseph Mbwilo na Silvanus Ngata ambaye naye ni mkuu wa
chuo hicho tawi la Tabora,
Akizungumza na waandishi wa
habari mda huu,Jijini Dar es Salaam,Waziri Kairuki amesema amefikia hatua hiyo
ya kuwasimamisha kazi watu hao ni baada ya kubaini kuwepo na uendeshaji usio ridhisha katika vyuo hivyo,
Amesema, Nassoro amemsimisha kazi baada ya
kushindwa kuwasimamia watumishi wa chini yake katika chuo hicho na pia kuwa na usimamizi usio na
ufanisi,
Amesema kuwa uzembe huo uliofanywa na Nassoro
umepelekea hadi matawi ya vyuo hivyo kuathirika .
“Mwaka 2011 hadi 2013 bwana Silvanus Ngata
aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la chuo cha Mtwara tofauti na ile fedha
iliyopangwa,na hata ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali ilithitisha ubadhilifu
huo ,
“Lakini huyo Nassoro baada ya
kugundua kosa hilo alimwamisha bwana Ngata na kumpeleka tawi la chuo
cha Tabora na kuendelea na wazifa wake na huyo bwana Ngata kutokana na haya
hakufuta taratibu pia namsimisha kazi”amesema Waziri Kairuki,
Pia waziri Kairuki amesema
amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za chuo,
“Huyu
Mbwiro kwa mwaka 2013 alitumia vibaya fedha za ada za wanafunzi za kiasi cha
bilioni 1 kwa mwaka fedha mwaka 2014,lakini licha ya ubadilifu huyo,huyo
Nassoro alimteua bwana Mbwiro kuwa Kaimu mkuu wa chuo kwa upande wa
fedha,kwahiyo huyo bwana Mbwiro namsimiasha pia,”amesema Waziri Kairuki,
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati Waziri
Kairuki anawasimamisha watendaji hao,mmoja wa watendaji hao,Nassoro alikuwepo
kwenye mkutano huo na wanahabari huku akiwa hajui kinatakachotokea,mara baada
ya waziri Kairuki kutaja kumsimamisha kazi,alionekana kama mtu mwenye kupata na
mshangao huo akijizuia hali yake isionekane.
Post a Comment