UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM FIGISUFIGISU,WAVUNJIKA TENA ,POLISI WATANDA KILA KONA UKUMBI WA KARIMJEE,UKAWA WAHAHA.
mwambawahabari blog
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa tena k wa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA.
Tukio hilo la aina yake limetokea leo Jijini mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutaka kuaharisha uchaguzi huo kwa madai kuwa uchaguzi huo ume wekewa pingamizi mahakamani , jambo hilo likawachukiza madiwani wa UKAWA wakidai kuwa hawajapata barua kuhusu kesi hiyo.
Mara baada ya UKAWA kugomea hoja hiyo ndipo wakafikia hatua ya kutaka kufanya uchaguzi wenyewe huku wakisema ahadi ya madiwani kufanya uchaguzi imetimia na wakaomba waendelee kufanya uchaguzi huo.
Wakati wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo ukawa wenyewe ,ndipo Polisi zaidi ya 15 wakavamiaka ukumbi huo na kuwataka kuwakamata madaiwani wa ukawa ili waondoke ukumbini kuzuia uchaguzi usifanyike,jambo lilowachukiza tena ndipo Polisi wakaanza kuwatuliza madiwani wa Ukawa .
credit fulhabari
Post a Comment