UFISADI WA SHILINGI MILIONI 20 WAZUA TAFRANI MSIKITINI JIJINI DAR ES SALAAM
Waumini
wa dini ya Kiislam wakizozana nje ya Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo
eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam katika swala ya Ijumaa
leo mchana, baada ya kutokea tafrani ya waumini hao dhidi ya viongozi
wao ambao wanatuhumiwa kutafuna fedha zaidi ya sh.milioni 20
walizochanga kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
Muumini
wa Msikiti huo, Mbarouk Mohamed Makame (kushoto), akizungumza kuhusu
fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao. Kulia ni mmoja
wa wazee wa msikiti huo, Mzee Selasela.
Mzee
Selasela akionesha dari la msikiti huo lililochakaa ambapo fedha hizo
zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao zingesaidia kuufanyia
ukarabati.
Hapa mzee Selasela akionesha uchakavu wa kapeti.
Hapa akionesha vyoo vilivyo chakaa vya msikiti huo.
Mwonekano wa vyoo vya msikiti huo vinavyotumika.
Waumini wakiwa nje ya msikiti huo wengine wakiswali.
Waumini wakiwa mbele ya vibanda vya biashara vilivyopo nje ya msikiti huo. |
Watoto wa shule ya awali katika msikiti huo wakiwa na mwalimu wao (kulia)
…………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
TAFRANI
kubwa imezuka katika Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja
Vingunguti jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa msikiti huo
kudaiwa kutafuna zaidi ya sh.milioni 20.
Fedha
hizo imeelezwa kuwa zilichangwa na waumini wa msikiti huo kwa ajili ya
ujenzi wa msikiti mpya baada ya unaotumika kuchakaa.
Imamu
mkuu wa msikiti huo aliyetajwa kwa jina la Hamidu Mitanga alilazimika
kutoweka ndani ya msikiti huo baada ya kuendesha swala ya Ijumaa
iliyofanyika jana mchana kutokana na waumini kuwa na jaziba kufuatia
imamu huyo kutamuka kuwa hakuhitaji kuulizwa maswali yoyote kuhusu
upotevu wa fedha hizo na kuwa uongozi uliopo utaendelea kuwepo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi msikitini hapo Dar es Salaam leo mchana
wakati wa swala ya Ijumaa mmoja wa waumini wa msikiti huo Mbarouk
Mohamed Makame alikiri kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za waumini
zilizochangwa kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
“Suala
la upotevu wa fedha hizo lipo na limeleta changamoto kubwa kwa waumini
na kusababisha kuwepo kwa makundi mawili moja likiwa lile
linalolalamikiwa kutafuna fedha hizo na lile linalotaka fedha hizo
zitolewe maelezo zilipo” alisema Mzee Makame.
Mzee
wa msikiti huo na Mwenyekiti wa Kamati ya watu 10 Saidi Ngubi alisema
fedha zinazoshindwa kutolewa maelezo ya matumizi yake na viongozi wa
msikiti huo zilitokana na mradi wa maji na michango ya waumini.
“Mimi
ndiye niliyeanza kuuliza matumizi ya fedha hizo lakini viongozi hao
wakawa hawana majibu na badala yake waliivunja kamati yetu na kuchagua
nyingine jambo lililoleta sintofahamu” alisema Ngubi.
Imamu
mkuu wa msikiti huo Hamidu Mitanda alisema fedha hizo zilitumika kwa
ajili ya mchakato mzima wa kupata umiliki wa kiwanja ulipo msikiti huo
na michoro ya ujenzi wa msikiti mpya na kuwa yeye ndiye aliyeanzisha
mpango wa kupata msikiti ulio bora na si bora msikiti.
“Binafsi
sina shida na cheo hiki cha Uimamu kwani nina shughuli zangu nyingi
mkitaka kuniondoa fuateni taratibu kama zili zilizoniweka madarakani na
sisi kama viongozi dhamira yetu ni kuwa na msikiti uliobora wa ghorofa
na si bora msikiti” alisema Mitanga.
Mitanga
alisema chokochoko hizo zilianza tangu mwaka 2007 ambapo tulikubaliana
kila muumini kati ya waumini 205 achangie sh.5000 za ujenzi lakini
waliochangia walikuwa ni waumini wachache ambapo zilipatikana sh.milioni
moja tu.
Imamu
huyo alisema uongozi unaoendesha msikiti huo hauko tayari kuachia
madaraka kwa tuhuma hizo ambazo hazina ukweli alizodai zinachochewa na
baadhi ya waumini.
Post a Comment