Ads

Naibu Waziri Annastazia aitaka jamii kutoa elimu ya Unyago kwa kuzingatia umri.

Na Shamimu Nyaki 
 mwambawahabariblog
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura amezitaka jamii kutoa elimu ya jando na unyago kwa kuzingatia umri na wakati sahihi wa mafunzo hayo ili kuweza kuondoa tatizo la mimba na ndoa za utotoni.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam  wakati alipozungumza na Wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka mkoani Mtwara wanaoshughulika  na mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni zinazosababishwa na utekelezaji wa wa mila na desturi hizo  mkoani  Mtwara.
“Ni vizuri   kuwafundisha watoto wetu maadili mema wakiwa wadogo,lakini ni vizuri Kuandaa namna ya kutoa elimu kwa kuzingatia umri na aina ya elimu ili kutoa taaluma hiyo kwa watu sahihi na wakati unaofaa. Alisema Mhe.Anastazia.”

 Mwenyekiti wa asasi hizo Dkt.Lillac Malumbo akitoa taarifa ya jinsi wanavyoshughulikia tatizo hilo amesema  kuwa asasi zinatoa mafunzo mbalimbali  kwa kwa wakufunzi  wa watoto wa kike ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni linalosababishwa na  utekelezaji wa mila mbalimbali mkoani   Mtwara.

“Tunaamini kuwa jamii   ikielimishwa kuhusu madhara yatokanayo  na  baadhi ya mada zinazotolewa katika mafunzo ya unyago na ambazo  zinaleta ushawishi kwa watoto wa kike kujiingiza katika zinaa, mimba na ndoa za utotoni tatizo ili  litaisha.Alisema Dkt. Lillac.”

 Dkt Lillac   ameongeza kuwa kuweka ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na  asasi hizo kutamuwezesha mtoto wa kike  kupata elimu, kuepuka magonjwa ya Zinaa ,kupunguza watoto yatima na watoto wa mtaani.

Hata hivyo mila hizi  zimekuwa zikiwanyima watoto wa kike haki ya kupata elimu kwa wakati, kusikilizwa, kuendelezwa na  kuwafanya  kubaki  tegemezi  kwa  muda  wote. 

Asasi hizi  zinatoka katika wilaya nne za mkoa wa Mtwara ambazo ni Tawaso Masasi,Msoapo Mtwara,Aware Mtwara vijijini ,Chakumuma Masasi,Nyerere Tandahimba,Kimweso Mtwara vijijini, pamoja na Children  Youth Development Innitiatives (CYDI).

No comments