Mawaziri wasisitizwa kurudisha Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma Kwa Viongozi.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majliwa Majaliwa (kulia) akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki.
Na. Immaculate Makilika
mwambawahabariblog
Baadhi ya Mawaziri na
Manaibu Waziri wasiorudisha fomu za Tamko la
Rasilimali na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu wamesisitizwa
kurudisha fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni katika ya
Ofisi ya Tume ya Maadili iliyopo jijini Dar es salaam na
watakaoshindwa kufanya hivyo watakua wamejitoa wenyewe kwenye nafasi zao.
Kauli hiyo imetolewa leo
na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majliwa
ofisini kwake alipokutana na Waandishi wa Habari akiwa ameambatana na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah Kairuki, ambapo ameeleza kuwa, kufuatia Semina iliyofanyika
Februari 25 mwaka huu kati yake na Mawaziri kuhusu Mwongozo
wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu, ambapo
Kamishna Mkuu, Mhe. Jaji Mstaafu Salome Kaganda alitoa maelezo kwamba kuna
baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao hawajarudisha fomu hizo hadi
kufikia jana.
Akiwataja Viongzoi hao,
Mhe. Majaliwa alisema kuwa, Mawaziri ambao hawajarudisha fomu hizo ni akiwemo,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. January Makamba, ambao wote
hawajarudisha fomu za Rasilimali na Madeni na fomu za Ahadi ya Uadilifu,
vilevile Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga ambaye hajarudisha fomu
ya Ahadi ya Uadilifu, na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako, ambaye hajarudisha fomu ya Tamko la
Rasilimali na Madeni, pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. Luhaga Mpina ambaye hajarudisha fomu zote
mbili.
Mhe. Majaliwa,
amewasisitiza Mawaziri hao kujaza fomu hizo kwa kua ni agizo la Mheshimwa Rais
kujaza fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni, “viongozi watakaoshindwa kutoa
Tamko la Rasilimali na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu
wanatakiwa kujieleza kwa kutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo na
watachukuliwa hatua” alisema Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa kifungu
cha 9 Sheria ya Maadili ya Uongozi wa Umma ya mwaka 1995 sura ya 8 inawataka
viongozi wote wa umma kujaza fomu za kanuni za Maadili ya
Viongozi wa Umma (Tamko la Raslimali na Madeni) na fomu ya Ahadi ya Uadilifu
mara wanapoteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi. Lengo la kujaza fomu
hizo ni kuwa na uwajibikaji kwa kiongozi juu ya uadilifu wake wakati wote
anapokua mtumishi wa Umma.
Post a Comment