Ads

LHRC Wamtaka Mwenyekiti wa ZEC Kujiuzulu Mara Moja..Chama cha CCK Chamvua Uanachama Katibu Wake Aliyetangaza Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

mwambawahabari

Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimemtaka Mwenyekiti wa tume ya 

uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha ajiuzulu wadhifa huo kutokana na hatua 

aliyochukuwa ya kufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya kurudiwa bila kufuata 

sheria hivyo kumemuondolea sifa ya kusimamia na kuongoza tume hiyo.


Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu MkurugenziMtendaji wa 

LHRC Bi Imelda Lulu Urrio ambapo amesema ukosefu wa taarifa sahihi na 

rasimi za 

michakato ya maridhiano toka kufutwa kwa uchaguzi kunaondoa imani ya 

wananchi juu ya viongozi wao, tume na mchakato mzima wa chaguzi za 

kidemokrasia Zanzibar.


Amesema kuwa kufutwa na kutangazwa upya kwa uchaguzi wa Zanzibar 

kunakiuka katiba,sheria,na kanuni za uchaguzi na pia misingi ya demokrasia ya 

utawala wa  sheria nchini.


Amesema kuwa katiba ya Zanzibar na sheria za uchaguzi hazijampa mamlaka 

mwenyekiti na hata tume yote kufuta uchaguzi na hivyo kilichotokea Zanzibar 

kimeaacha watanzania wakiwa hawaelewi ni sheria na katiba ipi imetumika 

kufuta 

uchaguzi huo.



Bi Imelda ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 123 cha sheria ya 

uchaguzi Zanzibar mtu akishachaguliwa uchaguzi wake hautohojiwa isipokuwa 

kwa kupeleka shauri mahakamani,hivyo kwa msingi huo LHRC wanaona 

kwamba 

hakuna kifungu chochote cha sheria kinachoipa tume ya uchaguzi au mwenyekiti 

wake mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamuru marudio isipokuwa kwa amri ya 

mahakama.


Wakati huohuo chama cha kijamii CCK kimemsimamisha kazi na uanachama 

naibu katibu mkuu wake wa Zanzibar Ali Khatib Aliambaye pia alikuwa 

mgombea urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi uliotangazwa kufutwa na ZEC 

Oktoba 2015.


Mwenyekiti wa CCK Costantine Achitanda amesema chama kimefikia maamuzi 

hayo ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufuatia uamuzi wake binafsi wa 

kutangazia 

umma kuwa CCK itashiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar kinyume na 

taratibu za chama.
Wakili Hamis Mkindi kutoka LHRC akiongea.Kushoto  ni  kaimu mkutugenzi wa 

kituo cha sheria na Haki za binadamu Bi Imelda Lulu Urrio

No comments