KILIO CHA LHRC TBC KUTO ONYESHA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA

Hata hivyo,LHRC pia wamelaani vikali kitendo cha Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo,Nape Nnauye kwa hatua ya kulifungia Gazeti la Mawio wakidai ni muendelezo wa kuminya uhuru wa habari nchini
www.mwambawawahabari.blogspot.com
Alipo zungumza na waandishi wa habari mwishon mwajuma jijini Dar es Salaam, kaimu mkurugenzi wa kituo hicho IMELDA LULU URIO amesema kuwa kusitishwa kwa matangazo ya bunge na chombo ambacho ni cha umma ni kuonyesha dhahiri kuwa serikali haina nia ya dhati ya kuheshimu yaki ya kupata habari ya kikatiba.
Alisema kuwa sababu zilizotolewa na waziri mwenye dhamana ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh NAPE NAUYE kuwa kusitishwa kwa matangazo hayo kunalenga kupunguza gharama za uendeshaji ni sababu ambazo zinaleta maswali kuwa gharama hizi ni za nini?,na kwa ajili ya nini?na zikitumika ni kwa manufaa ya nani?,na mchangiaji wa gharama hizi ni nani?huku akisema kuwa TBC ni chombo cha Umma hivyo kunawajibika kwa wananchi wote bila kujali gharama.
kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa inayohakikisha upatikanaji wa taarifa ikiwa ni pamoja na ule wa OPG –Open government partnership ambao ni jukwaa la serikali zenye uwazi mkataba ambao una misingi ya uwepo wa uwazi,ushiriki,wa wananchi,uwajibikajina uweledi na ubunifu wa kutumia Tehama.
Urio alisema kitendo cha waziri Nape kulifungia Gazeti la Mawio kunazidi kuiweka serikali ya magufuli kati mfumo wa kidikteta ambao unaonyima uhuru wa kutoa maoni ambao katiba ya nchi imetoa.
Alisema kuwa LHRC inaitaka serikali kutekeleza kwa vitendo maazimio ya makubaliano ya kimataifa na kikanda katika kulinda haki ya kupata habari na kufuta sheria kandamizi zenye kuminya uhuru huu kwa mfano sheria ya magazeti na sheria ya makosa ya mitandao na kutunga sheria wezeshi.

Pia LHRC wameitaka serikali kuacha kuminya haki za watanzania ya kupata habari za bunge kwa kisingizio cha gharama,na kutenga rasilimalin nyingi kuwezesha shirika hilo waweze kuonyesha moja kwa moja matangazo ya bunge.
Tangazo la kutokuonyeshwa kwa bunge kupitia TBC lilitolewa bungeni na waziri wa Habari NAPE NAUYE na baadae jana waziri mkuu Mh KHASIM MAJALIWA alitoa msisitizo kuwa wameamua kusitisha matangazo
Post a Comment