SERIKALI YAWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA KAMBI WA WAZEE NUNGE KUSITISHA UJENZI
mwambawahabariblog
Na. Magreth
Kinabo
mwambawahabariblog
Serikali imewataka
wananchi waliovamia eneo la kambi ya kuwalea wazee walioathirika na ugonjwa
wa ukoma yaliyopo Nunge Kigamboni, kusitisha mara moja ujenzi wa nyumba zao ama
kubomoa wenyewe ndani ya siku 21 kabla hatua ya kubolewa haijachukuliwa.
Agizo hilo limetolewa na
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii wazee na watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla, wakati alipowatembelea jana na kukuta idadi kubwa ya nyumba za
wananchi mbalimbali zilizojengwa ndani ya ardhi ya makazi hayo ya wazee.
Kufuatia hali hiyo ,Dkt.
Kigangwalla amemuagiza Mkuu wa kambi hiyo ya wazee Moses Gunza kutoa notisi ya
kusitisha ujenzi na ikiwezekana wananchi hao wabomoe wenyewe nyumba zao kabla
Serikali haijafika kuwabomolea.
“Hivi kweli watu wanaona
kabisa makaburi haya watu wamezikwa hapa tangu enzi za mjerumani halafu
wananunua na kujenga haiwezekani kuchezewa kiasi hiki watu wafike sehemu
waiheshimu Serikali na kufuata sheria za nchi,”alisema Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangalla eneo
hilo la Nunge limewekwa kwa ajili ya kulea na kuhudumia watu waliokuwa
wakiuugua ugonjwa wa ukoma sasa iweje ajitokeze mjukuu wa kati ya wazee hao
awauzie watu na ardhi hiyo huku akidai kuwa eneo hilo ni mali yake iliyotokana
na urithi wa babu yake jambo ambalo sio kweli.
“Ninatoa siku 21 watu
hawa wote waliojenga katika makazi haya ya wazee kusitisha mara moja ujenzi wa
nyumba zao au kubomoa na hiyo mtu anayedai eneo hili ni lake akija hapa akatoa
maagizo yake mnipe taarifa nitamuweka ndani.,”alisema Dkt. Kigwangalla.
Akipokea akigizo hilo
mkuu wa kambi hiyo Moses Gunze alisema wananchi hao walikwisha pewa notisi
tangu mwaka jana 2015 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kuwataka wananchi
waliopo eneo lote la Nunge kusitisha zoezi la kuendelea kujenga nyumba zao
agizo ambalo halikutekelezwa kutokana na muingiliano wa kisiasa.
“Hawa watu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali alishatoa stop order
kuwataka wasiindelee na ujenzi wowote
hapa lakini baadaye wananchi hawa wakajipanga wakaenda Bungeni Dodoma na
baadaye aliyekuwa Waziri wa afya Dkt. Seif Rashid akatoa barua akasimamisha
zuio matokeo yake watu wakaendelea kujenga tena, ’’alisema Moses.
Kwa upande wake mzee
Salumu Ubwabwa ambayea ameathirika na ukoma anayelelewa katika kituo hicho
amebainisha kuwa kuna anayejulikana kwa jina la Bahari Seifu anayewauzia watu
viwanja akidai kuwa eneo hilo la Nunge ni lake amerithi kutoka kwa babu yake
Mohamedi Sheweji.
Mzee Ubwabwa amebainisha
kuwa yeye amefika katika makambi hayo tangu mwaka 1984 baada ya kuugua ukoma
kutokana na miaka hiyo watu wa ukoma kutengwa mjerumani akawajengea jumba la
mabati na kuwahifadhi huko Kigamboni ili wasiweze kuvuka kwenda ng’ambo kwani
wangeweza kusababisha maambukizi.
Alisema mwaka 1974 Rais
wa kwanza Hayati Julius Nyerere aliwajengea nyumba hizo na Serikali ya Tanzania
ikaendelea kuwatunza hadi sasa.
Mzee Ubwabwa alisema
katika makambi hayo alikuwepo na mzee Mohamedi Sheweji ambaye naye alikuwa
mgonjwa wa ukoma alihifadhiwa kwenye makambi hayo hivyo anashangaa kuona Bahari
Seif akijitokeza hivi sasa na kuanza kuuzia watu viwanja kwa madi kuwa ardhi ya
Nunge ni uridhi wa babu yake wakati si kweli.
Post a Comment