TAASISI YA PASS TRUST FORUM YAFANIKIWA KUTOA DHAMA YA TRILIONI 2.4 SEKTA YA KILIMO
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam
KATIKA kuhakikisha Sekta ya Kilimo nchini inaimarika Taasisi ya PASS Trust Forum imeweza kutoa dhamana ya takribani shilingi trilioni 2.4 katika kipindi cha miaka 25 ,Aidha, tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,kwani serikali imeongeza uwekezaji wa shilingi trilioni 1.2 katika sekta ya kilimo, hususan kwenye bajeti ya kilimo cha umwagiliaji.
"Sisi tunaweka dhamana ambapo tunamuweka mkulima mbele tunachochakupoteza mkulima akikopeshwa asilipe na hivyo dhamana yetu inakwenda hadi asilimia 80 katika sekta ya kilimo,uvuvi na mifugo,ni kwamba tunampeleka mkulima mbele tunamtengenezea mpango biashara na mpango biashara huu tunaunganisha na taasisi,tunaweka mbele fedha taslimu ambayo inafikia kiwango asilimia 80 ya mkopo wake halafu tunaiambia taasisi ya fedha imkopeshe katika gurudumu hili la sekta katika kilimo,mifugo ,uvuvi na mkulima akafeli PASS Trust tunapoteza Ile asilimia 80 ya dhamana",amesema Kamanda
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Oktoba 13,2025 katika maadhimisho ya miaka 25 ya PASS Trust Business Forum yanayofanyika Jijini Dar es Salaam,Mwakilishi wa MkurugenziMkuu za PASS Trust na Mkurugenzi wa Biashara, Adam Kamanda amesema kwamba taasisi hiyo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Denmark, ikiwa na lengo la kuchochea kilimo biashara, ufugaji, uhifadhi wa misitu na kuongeza uwekezaji kupitia taasisi za kifedha.
Kamanda amebainisha kuwa kongamano hilo limeunganisha mikoa ya Pwani, Dar es Salaam,Morogoro, Dodoma na Zanzibar, likiwaleta pamoja wadau kutoka taasisi mbalimbali za fedha nchini.
Pia amesema kongamano hili limefanikiwa kufanyika katika mikoa ya Njombe, Arusha, Kahama, Moshi na Bukoba ili kujadili fursa na changamoto zinazowakabili.”
Kwa upande wake, Daniel Sumpo kutoka Equity Bank, alieleza kuwa wakulima wadogo wanakabiliwa na ugumu wa kupata mikopo. Kupitia PASS Trust Business Forum, benki hiyo imekuwa ikitoa garantii kwa wakulima ili waweze kupata mitaji na nyenzo bora za kilimo, hivyo kuongeza tija katika uzalishaji.
Naye Meneja Mahusiano kutoka Benki ya Washirika Makao Makuu Dodoma ,Hadija Seif amesema ushirikiano wao na PASS Trust umeleta mafanikio makubwa kwa wakulima.
Hata hivyo kumekuwa na changamoto za masoko,pembejeo na elimu ya kilimo kama vikwazo vinavyohitaji kushughulikiwa kwa haraka.
Maadhimisho haya yameonesha dhamira ya dhati ya PASS Trust Business Forum katika kuimarisha sekta ya kilimo kupitia ushirikiano wa taasisi za fedha, serikali na wadau wa maendeleo. Kwa kuwepo kwa mazingira wezeshi na bajeti madhubuti, Tanzania ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wake kupitia kilimo endelevu.

.jpeg)
.jpeg)

Post a Comment