Ads

NEEC YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI WA MKOA WA DAR KUHUSU UWEZESHAJI KIUCHUMI






Na Mwandishi wetu


Dar es Salaam 

BARAZA la  Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kiuchumi kwa lengo la kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu majukumu ya baraza hilo na jinsi linavyotekeleza shughuli zake za uwezeshaji wananchi kiuchumi.


Akizungumza kwenye ufunguzi wa semina  ya wanachama wa JOWUTA leo Oktoba 10,2025 Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa NEEC, Neema Mwakatobe amesema kwamba baraza linatambua  mchango mkubwa wa vyombo vya habari kuelimisha jamii hivyo kupitia ushirikiano wa waandishi ,wananchi watapata nafasi ya kufahamu kwa undani namna NEEC inavyoratibu shughuli za uwezeshaji kiuchumi pamoja na fursa zinazotolewa kwa watanzania kushiriki katika uchumi wa nchi


Amesema kwamba NEEC iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na jukumu lake kuu ni kufaiatailia na kutathimini shughuli zote za uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini


Aidha amesema kwamba Sera ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ilianzishwa mwaka 2004 na Sheria ya mwaka 2005 za ilianzishwa rasmi na Baraza Hilo kwa madhumubi ya kuratibu,kufuatilia na kuhakikisha wananchi wanashiriki katika shughuli kiuchumi


Pia amesema ni wajibu wa NEEC kiafahamu wadau wote wanatekeleza shughuli za uwezeshaki na kutoa taarifa kwa umma kuhush fursa zilizopo ili wananchi wapate taarifa

 sahihj za uwezeshaji


Naye Katibu wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya habari(JOWUTA) Sulemani Msuya amewashukuru NEEC k2a kutoa elimu hiyo kwa wanachama wao,kwani elomu hiyo itatoa uelewa mpana kwa wanahabari kuhusu majukumu na shughuli zinazofanywa na Baraza Hilo.


Ameeleza kwamba JOWUTA Ina wanachama zaidi ya 500 nchini kwa mkoa wa Dar es Salaam Ina wanachama zaidi 150,ameiomba NEEC kuendelea kutoa mafunzo kama hayo kwa wanahanari wa mikoa mingine ili kuendelea kueleimisha umma kwa usahihi.

"Tunaishukuru NEEC kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari,kupitia warsha hii wanachama wetu watakuwa mabalozi wazuri wa kufikisha taarifa za uwezeshaji kwa wananchi,"amesema  Msuya


Katika mafunzo hayo wanahabari wameweza kujifunza mada nne zilizowasilishwa na watoa mada kama ifuatavyo.

1. Mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi


2. Ushiriki wa Watanzania katika uchumi


3. Utoaji wa huduma za biashara


4. Muongozo wa watoa huduma za biashara

No comments