Ads

BASHUNGWA AENDELEZA KAMPENI ZA KUSAKA KURA ZA DKT. SAMIA - KARAGWE

 






Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Innocent Bashungwa, ameendelea na kampeni za kuomba kura za Mgombea wa Urais, Ubunge na Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Karagwe kwa kueleza kuwa CCM ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuendelea kuongoza Serikali bila nchi kuingia kwenye machafuko.


Bashungwa ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika kijiji cha Nyakayanja, Kata ya Nyaishozi, ambapo alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu kwa kujitokeza kupiga kura za Ndiyo kwa wagombea wa CCM ifikapo Oktoba 29.


Akiomba kura za Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bashungwa alisema; “Zamu hii akina mama ni zamu yenu. Huyu ni mama mwenzenu, naomba mpende, tumpe ushirikiano na kura zote za akina mama ni mtaji namba moja.”


Aidha, Bashungwa alitumia mkutano huo kuomba kura zake kama Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe pamoja na kura za Mgombea Udiwani wa Kata ya Nyaishozi, Wallace Mashanda, ambapo ameahidi kuendelea kuboresha huduma za kijamii, ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara zinazounganisha vijiji mbalimbali katika jimbo hilo.

No comments