Ads

CIP YAFANYA UTAFITI KURA ZA MAONI NA KUBAINI ASILIMIA 84.5 KUPIGIA KURA MGOMBEA WA CCM UCHAGUZI MKUU




Na Angelina Mganga

Dar es Salaam 

KITUO cha Sera zs Kimataifa-Afrika kwa kiingereza Centre for International Pilicy-Africa(CIP -Africa) mnamo Septemba 30  Hadi Oktoba 5,2025 kimefanya utafiti  kisayansi unaohusisha  kura za maoni kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29 na  takwimu inaonyesha zaidi ya watu 1,976 wamehusishwa katika utafiti huo wakiwemo wanaume 988 na wanawake 988 sawa na uwiano wa asilimia 50 na umri Kati Yao wenye miaka 18 hadi 25 sawa na asilimia 29.


Akizungumza na waandishi wa habari Leo Oktoba 22,2025,Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji wa CIP, Thabit Mlangi amesema kwa mujibu wa taarifa ya kura ya Maoni ya Uchaguzi Mkuu ya  CIP imeeleza kuwa katika Vyama (18) vitavyoshiriki Uchaguzi Mkuu  vimefanikiwa kusimamisha wagombea katika nafasi ya urais,Ubunge na udiwani .Vyama hivyo ni ikiwemo Chaumma ,CCM, ACT-Wazalendo, CUF,SAU, UDP,Makini,NLD,NCCR-Mageuzi,NRA,AAFP,UPDP,ADA-TADEA,D,TLP,CCK,ADC na DP ripoti hiyo ilieleza kuwa watu 1,976 walihojiwa.


Aidha,  amebanisha kuwa kati ya watu hao, asilimia 81 waliweza kujipambanua kuwa wanafuatilia michakato ya kisiasa nchini wakati asilimia 19 wamekuwa sio wafuatiaji wa mchakato huo.


Utafiti huo umebainisha kuwa Wanaume wamekuwa wakiongoza kwa ufuatiliaji  mchakato huo kwa asilimia 57 huku Wanawake ni 43.


"Katika kundi la wafuatiaji kwa ngazi ya elimu ya msingi ni asilimia 19, Sekondari ,ni asilimia 55, huku wenye elimu kwa ngazi ya Chuo ni asilimia 26"imesisitiza taarifa hiyo.


Amebainisha kwamba wa upande wa ushiriki wa mikutano  idadi ya Ushiriki imefikia asilimia 53 huku wahudhuriaji kwenye mikutano ya Kampeni ni 76 waliweza kuhudhuria mikutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM  wakifuatiwa na Chaumma  kwa asilimia 15.


" Baadhi ya  wananchi waliohojiwa kuhusu Rais ajaye ashughulikie Nini kwenye vipaumbele vya taifa, taarifa hiyo ilieleza kuwa Wananchi walipenda Kiongozi ajaye ashughulikie Maji,(78) Elimu (78) Miundombinu (69) huku suala la Rushwa ni asilimia 60" 


Pia amesema mikoa iliyofanyiwa kura ya maoni ni Arusha,Dar es Salaam,Dodoma,Geita,Iringa,Kagera,Kaskazini Pemba,KaskaziniUnguja,Kigoma,Kilimanjaro,Mara,Mbeya,Morogoro,Mtwara,Mwanza,Pwani,Ruvuma,Tabora na Tanga.


Kuhusu kushiriki kupiga kura Oktoba 29,2025 asilimia 83 ya washiriki kura ya maoni wamethibitisha kupiga kura ,huku kura za maoni ya urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika asilimia 84.5 wanaonyesha kuwa watampigia kura mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) na asilimia 8 walibainisha kwamba kura yao ni siri 

ao.

Sanjari na hayo,Kituo hicho kimezishukuru mamlaka za serikali kuu na serikali za mitaa kwa kuunga mkono kura hii ya maoni ambayo ni sehemu ya ustawishaji demokrasia.


Alimalizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kupiga kura tarehe 29,Oktoba 2025,kwa amani na utulivu kama kauli mbiu inavyoeleza"Kuna maisha baada uchaguzi

No comments