MECHI ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga  imemalizika kwa kutosha nguvu ya bila kufungana mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Timu zote zimecheza mchezo mzuri dakika zote mbili hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho watani hao wamegawana alama moja moja.

Kwa Matokeo hayo Yanga wameendelea kuongoza Ligi hiyo kwa kufikisha Pointi 20 huku Simba wakibaki nafasi ya pili kwa pointi 18 baada ya timu zote kucheza mechi nane.

Pamoja na hayo itakumbukwa kuwa Watani hao  mwaka huu wamekutana mara Tano Yanga Ikishinda mara Tatu  Simba mara moja na Leo Timu zimetoshana nguvu, huku mashabikibwa Simba Katika uwanja wa Mkapa  wakionekana kushangia Zaidi matokeo ya Leo .

"Naitwa  Ally Musa nishabiki wa Simba  kindaki ndaki , nashangila matokeo ya Leo kwakuwa  mwanzo wa mchezo Yanga walikuwa wanapewa nafasi kubwa  ya kushinda , nakweli ukiangalia sisi Simba hatunatimu nzuri msimu huu ukilinganisha na wenzetu " Alisema shaki huyo