Ads

SERIKALI YAPONGEZA MAENDELEO YA MRADI WA FISH4ACP ZIWA TANGANYIKA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi, Dkt. Rashid Adam akizungumza jambo katika warsha kuhusu  mnyoro  wa thamani wa dagaa na mgebuka wa Ziwa Tanganyika pamoja na kujadili maendeleo ya mradi FISH4ACP iliyofanyika Mkoani Kigoma.

...............

Serikali imetoa pongezi kwa wachambuzi wa mnyororo wa thamani kwa kazi ya kuboresha uchambuzi wa mnyoro wa thamani huku ikisifia mradi wa FISH4ACP .

Akizungumza mjini Kigoma katika warsha juu ya kukuza mnyoro huo katika  dagaa na mgebuka wa Ziwa Tanganyika nchini , Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi, Dkt. Rashid Adam, amesema kuwa lengo ni kuwa na ustawi wa kiuchumi na uzalishaji wa ajira kwa kuhakikisha uendelevu kiuchumi na kijamii.

"Mijadala umezingatia kupata mpango bora utakao tekelezeka ili kuchangia ajira pamoja na malengo ya kitaifa na kimataifa,"amesema Dkt. Adam.

Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka huu Benki ya NMB tayari imeanza kuvitambua vikundi vyenye uitaji ili kuweza kuvikopesha 

Katika mchakato huo mpana juu ya kukuza mnyororo huo wa thamani wa Ziwa Tanganyika Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismaili Kimirei, amesema kuwa FISH4ACP wamekuwa wadau katika mpango wa utekelezaji wa mkakati wa maboresho 2021 - 2024.


"Mradi wa FISH4ACP ambao umekuwa utekelezwa kwenye nchi 12 unafadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) na serikali ya ujerumani unagharimu kiasi cha Euro milioni tatu" amesema Dkt. Adam.

Mvuvi katika Mwalo wa Katonga Bw  Francis John,  amesema kuwa mradi huo utawezesha kukua kwa soko la samaki katika ziwa hilo, ambapo tayari samaki wake  wapo katika  soko la nje, nchi za Australia pamojo na  Marekani wamekuwa ni wateja katika soko.

No comments