Ads

BULAYI : MRADI WA FISH4ACP ZIWA TANGANYIKA UTAZINGATIA UTAALAM.

Wadau kukuza mnyoro wa thamani Mkoani Kigoma wamefanya wasilisho na mjadala wa wazi kuhusu rasmu ya utekelezaji na mipango ya wazi.

Katika hatua hiyo kwa pamoja Mnyororo wa thamani wa dagaa, lumba na Mgebuka wa Ziwa Tanganyika ndiyo uliolengwa kufanyiwa uchambuzi wa mnyororo huo.

Akizungumza katika warsha iliyofanyika kwa muda wa siku mbili katika kujenga mijadara iliyokuwa na maono  Makuu Mkoani humo, Mkurugenzi Idara ya Uvuvi ,Wizara ya Mifugo na Uvuvi Emanuel Bulayi,  amesema kuwa kupitia mradi wa FISH4ACP nchini utakuwa suluhisho chanya.

"Kwa taarifa nzuri mradi huu, unakuja na mipango inayotekelezake, hivyo watafiti watakuwa wanazingatia utaalam wao ,"amesema Bw. Bulayi.

Kupitia njia ya mtandao washiriki wengine waliweza kushiriki warsha hiyo, ambapo muundo wa mkutano huo ulihusisha wadau kukutana ana kwa ana, huku Bw. Adam Sendall  kutoka (FAO) nchini Italy aliweza kushauri .

"Njia itumike kuweza kuwabaini wateja katika masoko yanayoweza kuboreshwa, huku nguvu kubwa ikiwa ni kuwekeza katika usalama wa chakula kwa mlaji,"amesema Bw. Adam.

Bw. Adam amesema hayo ni maono juu ya shughuli maalum katika uwekezaji unaohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati wa maboresho .

Bw. Elias Ndagama mvuvi kutoka Mwalo wa Katonga Mkoani Kigoma amesema kwa sasa ni muda mwafaka kuwa wanaitaji huduma za usaidizi kwa kukuza mnyoro wa thamani.

" Moja ya changamoto zinazotukabili mradi huo kuweza kuboreshewa kwa maeneo yao katika kupatiwa miundo mbinu ya kisasa,"amesema Bw. Ndagama.

Imeelezwa kuwa FISH4ACP ni mpangao wa Umoja was Mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) unaochangia usalama wa chakula na lishe, ustawi wa kiuchumi na uzalishaji wa ajira na kuhakikisha uendelevu wa kiuchumi, kijamii na kimazingira wa mnyororo wa thamani wa uvuvi na ufugaji wa viumbe maji katika Afrika Karibiani na Pasifiki.

Mradi huo unajipambanua kutekelezwa na Shirika la Chakula na Kilimo Cha Umoja wa Mataifa (FAO) kwa Ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU), huku mshirika wa kitaifa nchini  akiwa ni (TAFIRI).

No comments