RC MAKALLA AZINDUA MKAKATI WA USAFI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA DAR.
..........
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amewataka
watendaji wote wa mkoa huo kusimamia majukumu yao kwa vitendo ikiwemo
kuwasimamia wafanyabiashara wadogo wadogo 'Wamachinga' kwenda kwenye maeneo
waliohamishiwa pamoja na kuzingatia mazingira yakuwa safi.
Akizungumza leo
jijini Dar es Salaam wakati akizindua mkakati wa usafi na uhifadhi wa Mazingira
uliobeba kauli mbiu isemayo Safisha
Pendezesha Dar es Salaam.
RC Makalla amesema kuwa kampeni ya kuwaondoa Wamachinga
katika maeneo yasiyoruhusiwa imeafanikiwa asilimia 90 na kwamba kauli ameitoa
kutokana na baadhi yao kuendelea kukaidi kuondoka kwenye maeneo hayo hivyo
ameziagiza manispaa kuwasimamia waende walikopangiwa.
" Da es Salaam tumefanikiwa kwa asilimia 90
kuwaondoa Wamachinga kwenye wasiotakiwa wale waliokuwa hawalitakii mema jambo
hili wameshindwa viongozi wao ndio waliosaidia kufanikisha hili," amesema
RC Makalla.
RC Makalla ametangaza kuwa kila Jumamosi ya mwisho wa
mwezi iwe siku ya kufanya usafi katika jiji hilo hivyo wananchi wanatakiwa
kushiriki pamoja na kuwaagiza Wenyeviti wa Mitaa kutimiza wajibu kwa
kuhamasisha usafi katika maeneo yao.
Amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuwa waratibu wa usafi
wa pamoja katika wilaya zao kwa kuweka ratiba ya wananchi kushiriki kufanya
usafi ili jiji hilo liwe hali ya usafi.
Maagizo mengine ni taassi za umma kulinda maeneo yao
kisheria ili wasivamiwe na Wamachinga, majengo yote umma, na binafsi kupigwa
rangi,manispaa zote kupitia sheria ndogondogo za ufanyaji biashara kiholela na
utupaji taka pamoja na kutoa vibali kwa kampuni za usafi zenye vigezo.
Amewaomba viongozi wa dini kuwahamasisha waamini wao
kufanya usafi kwani usafi haliufuati itikadi za kidini hivyo dini zote
zinahimiza suala hilo.
RC Makalla amebainisha kuwa Disemba 4 mwaka huu
wananchi jiji hilo watasherehekea miaka 60 ya uhuru muda wa asubuhi kwa kufanya
usafi katika maeneo yao na kwamba jioni kutakuwa na burudani katika Viwanja vya
Leaders, Kinondoni.
Katibu Tawala wa Mkoa huo, Hassan Rugwa amempongeza RC
Makalla kwa kuja na mkakati huo na kusisitiza tayari wameshaanda mikataba ya
utekelezaji wake.
Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
amewahimiza wakazi kumsaidia Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kushiriki kufanya usafi kwani dini zote zinasisitiza usafi.
Baba Askofu Jacob Sosthenes ametilia mkazo suala la
ufanyaji ni la waamnini wa dini kutokana maandiko ya vitabu vya dini kuwataka
wanadamu kuwa wasafi na kuhifadhi mazingira.
Mabalozi wa Mkakati huo akiwemo Msanii Ali Kiba, Rajab
Kahali' Harmonize' na Steve Nyerere wamempongeza RC Makalla na kumuhakikishia
kufikisha elimu ya usafi na uhifadhi mazingira kwenye jamii.
Msemaji wa Wamachinga wa Kariakoo Masoud Issa
amempongeza RC Makalla na kumuhakikisha wako tayari kuhamasisha wenzao
kushiriki kufanya usafi katika maeneo yao.
Amemuomba RC Makalla kutenga stendi za magari katika
maeneo waliyopelekwa Wamachinga ili wateja waweze kufika katika maeneo yao
kirahisi.
Post a Comment