Ads

WADAU WA GsI TANZANIA WAKUTANA KATIKA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 9.


Mwenyekiti wa Gs1 Tanzania Jumbe Menye amesema Gs1 Tanzania hufanya kazi Tanzania bara na Tanzania visiwani na huu ni mwaka wa tisa na mwaka wanatimiza mwaka wa kumi ikiwemo shughuli kubwa ya Gs1 ni kutoa alama kwa bidhaa  zinazozalishwa Tanzania. 

Membe amesema hayo leo Jijin Dar es salaam katika kongamano la maadhimisho ya miaka 9 ya Gs1 amesema Gs1 ikiwa katika kufanya kazi hiyo lakini pia inasaidia wachimbaji madini wanawake kwa kutoa semina mbalimbali  katika kuweza kusaidia kukuza uelewa zaidi wa shughuli hiyo ili kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Naye Mmoja kati ya wadau wa Gs1 Tanzania ambaye ni Mchimbaji wa madini mwanamke Naomi Tsubaki Nzullunge amesema wanawake wana mwamko wa kufanya kazi ili kujiingizia kipato kwa kufanya kazi mbalimbali ikiwemo ya uchimbaji madini.

Naomi amehamasisha wachimbaji wa madini wanawake kuhudhuria  kwenye semina zitolewazo na Gs1 ili kuendana na Kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Amesema wachimbaji madini Wanawake wapeane taarifa kuhusu Semina mbalimbali zitolewazo na Gs1 ili kusaidia wachimbaji wote Wanawake wanakuwa kipaumbele katika kutoa huduma bora ya shughuli hiyo.

Naomi pia anawapongeza Sana wachimbaji madini wanawake wengi kujitokeza kwenye uchimbaji na anawapongeza sana Gs1 kwa shughuli kubwa wanayoifanya kukuza maendeleo ya kichumi

No comments