Ads

SERIKALI YAFIKISHA ASILIMIA 94 KUSAMBAZA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO.

 

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele amesema serikali imeshambaza mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa asilimia 94 katika maeneo yote nchi nzima.

Aliyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la nne la Tehama nchini lenye kaulimbiu inayosema kuelekea mapinduzi ya nne ya viwanda ambapo mapinduzi hayo yanategemea kiwango cha juu cha Tehama yenye uwezo mkubwa wa kutatua changamoto na kuchangia Maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kamwele alisema kuwa mpaka sasa serikali imesajili kampuni 20 za mawasiliano na kampuni 87 zinazotoa huduma kwenye mtandao pia serikali inatumia tehema kwa kiasi kikubwa katika uendeshaji wa huduna na Mifumo yake mbalimbali ikiwemo malipo,barua pepe na e-ofice hivyo kurahisisha huduma kwa wananchi.

"Wapo vijana wengi wanasona IT NA ICT lakini wanakosa ajira, kutokana na tàasisi na wasau kutumia wataalamu kutoka nje,muda mwingine vijana wetu wanachukuliwa na mataifa mengine na wakigundua vitu mbalimbali na kunufaisha mataifa hayo,ni muhimu tukatumia vijana na kuwa nafasi kuonyesha ujuzi wao''alisema Waziri Kamwele

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano,sekta ya Mawasiliano Dr Zainabu Chaula alisema washiriki watabadilishana uzoefu na kuweza kuenda na kasi ya mavadiliko ya tehama katika kuchochea maendeleo ya jamii na kiuchumi.

"Tehama imeweza kurahisisha huduma za mawasiliano na huduma nyinginezo ikiwemo uuzaji wa bidhaa,usafirishaji na ukataji wa tiketi mbalimbali".

Nae Mkurugenzi mkuu wa tume ya tehama Mhandisi Samsoni Mwela alisema katika kongamano wamezindua rasmi mfumo wa kusajili wataalamu wa tehama ambapo wametoa vyeti 100 kwa watalamu ili kuweza kusaidia taifa kujua idadi yao na kutambua uwezo wa ndani ya nchi katika maswala ya tehama.

"Tehama inatumika katika sekta mbalimbali hivyo ni muhimili mkubwa katika kukuza uchumi,tehama inaweza kutumika katika sekta ya fedha,viwanda,kilimo,elimu na maeneo mengine mengi,tunahitaji kuboresha mkakati wa tehama". Amesema

No comments