Ads

WANANCHI WALIOWEKEZA MRADI WA KUKU WAMLILIA RAIS MAGUFULI



Mwamba wa Habari

 Wawekezaji waliowekeza  Katika  kampuni ya MR Kuku  Farm , wameiomba Serikali kuingilia Kati suala la kushikiliwa kwa account za kampuni hiyo ambapo   zaidi  ya watu   4500 waliowekeza katika mradi wa Kuku.

Wakizungumza na waandishi wa habari Katika mkutano uliofanyika Kigamboni wawekezaji hao wamesema , wakati wakiwekeza Katika kampuni hiyo waliona taratibu zote za kisheria zilifuatwa ikiwemo  TRA,OSHA,WCF,BRELA hivyo alishangazwa na kuona kuwa kampuni hiyo account zake zimeshikiliwa .

"Wengi tumeathirika wengine ndoa zimevujika ,uaminifu umepungua ,wengine waliwekeza ili kusaidia familia zao wengine niwagonjwa ,wengine ni wajane "Alisema Julius Talian.

Aidha wemeomba  Rais Dkt John Magufuli kuwasaidia ili waweze kuendelea na biashara yao ya ufugaji Kuku ,ama wapatiwe haki yao kwani wanahitaji hizo fedha kwaajili ya mahitaji yao ikiwemo kusomesha Watoto wao na kujiendeleza kibiashara.

"Nilishawishika kujiunga na kazi ya uwekezaji huu baada ya kuona Katika mitandao wakiwa wamejiunga Mashekhe wakubwa wakipromoti hii kampuni, nilifuatilia na kujiridhisha kuwa kampuni hii ilikuwa halali  kisheria nilifika hadi Katika Shamba la Kuku nikaona  wangu walikuwa  elf kumi , Ila sasa nashangaa kuona kuwa eti hii kampuni imehusishwa na tuhuma za utakatishaji fedha " Alisema Iddi Zubeiry .



 Mmoja wa wawekezaji ambaye amejitambulisha  kwa jina William Lyamusanyaga , mstaafu amesema  kamamstaafu aliwekeza kwa matarajio kuwa atafaidika na alikuwa akichukua fedha kupitia account ya Bank na sasa anashindwa kuwa saidia hata kuhudumia familia ambayo wengine ni yatima aliachiwa na marehemu mtoto wake naye amemuomba Rais Dkt John Magufuli aingilie kati hili suala liweze kuisha .


''Niliifahamu Mr Kuku kupitia Whatsap na baadaye nikaja kuonana naye na kujiridhisha kuwa yuko kisheria na nikajiunga kwa muda wa miaka miwili sasa  na nilipata faida mara kadhaa lakini baadye nika sikia kuwa account zinashikiliwa na baadaye akakamatwa  ila haya tunaiachia Serikali ijiridhishe kwa tuhuma hizo lakini sisi tunaomba kama wananchi wanyonge tachiwe mradi wetu kama kunakosa la mtu mmoja tusiumizwe na sisi watu waote 4500  kuna familia nyuma yetu zinatutegemea naomba Rais Magufuli utusaidie"Alisema Colins 


No comments