Ads

Maalim Seif afunguka kumuungamkono Tundu Lissu, Membe Apinga

  


Chama cha ACT-Wazalendo kimetangaza kumuunga mkono Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.


Msimamo huo umetolewa jana Jumatatu tarehe 21 Septemba 2020 na Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo katika mkutano wa kampeni za urais za chama hicho Zanzibar, zilizofanyika Jimbo la Donge.
 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Janeth Rithe, Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT-Wazalendo, Maalim Seif ameutumia mkutano huo wa kampeni kumuidhinisha Lissu kuwa mgombea wao wa urais badala ya Bernard Membe, aliyepitishwa na chama hicho kugombea nafasi hiyo.

Hata hivyo, Membe amepinga msimamo huo, akisema kwamba yeye ndiye mgombea Urais wa Tanzania wa ACT-Wazalendo, aliyekabidhiwa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Membe ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter, huku akisisitiza kwamba, taarifa zinazotolewa kwamba ACT-Wazalendo imeungana na Chadema kwenye mbio za urais si za kweli.


No comments