MWAKALINGA AKABIDHI VIFAA VYA MAFUNZO CHUO CHA UJENZI MOROGORO.
Mwambawahabari
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Arch. Elius Mwakalinga, amekabidhi mtambo mmoja (Grader) na Komyuta 20
kwa Uongozi wa Chuo cha Ujenzi Morogoro na kutoa wito kwa wazazi,
walezi, wafadhili na waajiri wote kuwapeleka vijana na watumishi wa
jinsia zote kupata mafunzo ya ufundi stadi ili kuweka uwiano mzuri kati
yao.
Wito
huo ameutoa mkoani Morogoro akiwa kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo
ambapo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu huyo amesema kuwa
hafurahishwi na kuwepo kwa idadi ndogo ya wanawake katika baadhi ya
kozi, Chuoni hapo.
"Nimesikitika
kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Chuo kuwa kozi nyingi zina idadi
kubwa ya wanaume kuliko wanawake na nyingine zina wanaume pekee, elimu
ya ufundi stadi ni kwa wote, shime jinsia zote kushiriki kupata mafunzo
haya", amesema Mwakalinga.
Katibu
Mkuu Mwakalinga, amefafanua kuwa utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa
vijana utatoa mchango mkubwa katika azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya kujenga uchumi
wa kati na wa viwanda ambapo fani za ujenzi ni muhimu katika kufikia
azma hiyo.
Aidha,
Mwakalinga ameupongeza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwa kukubali
kutoa mtambo mmoja (Grader) na Wizara kutoa kompyuta 20 ili vitumike
kufundishia wanafunzi ambapo amesema kuwa vifaa hivyo vitakuwa chachu ya
utoaji mafunzo hapo chuoni.
"Naamini
sasa kuja kwa vifaa hivi kutarahisisha na kuhamasisha mafunzo kwa
vitendo, nawasihi mtumie vifaa hivi kwa malengo yaliyowekwa pamoja na
kuvitunza vizuri", amesisitiza Katibu Mkuu Mwakalinga.
Sambamba
na hilo Katibu Mkuu Mwakalinga amesema kuwa Wizara ipo katika hatua za
mwisho za kuanzisha Taasisi ya Teknolojia yaUjenzi kwa kuunganisha Chuo
cha Ujenzi Morogoro na Chuo cha Teknolojia Stahiki ya Nguvukazi
kilichopo Mbeya ambapo amefafanua kuwa lengo la kuanzishwa kwa Taasisi
hiyo ni kuboresha mafunzo yanayotolewa na vyuo hivyo viwili.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Chuo cha Morogoro, Melkizedeck Mlyapatali amesema
kuwa chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa
watumishi wakiwemo wahandisi wa fani mbalimbali, wakufunzi, wahasibu na
wafanyakazi wengine kutokana na wafanyakazi wengi kustaafu kwa mujibu wa
sharia na wengine kufariki dunia.
Chuo
kina jumla ya wanafunzi 403 na kinaendesha mafunzo ya ufundi stadi na
masomo ya kawaida kwa lengo la kuwezesha wahitimu kuwa mahiri katika
Nyanja za ujenzi.
I need to know, which qualification is required to join chuo Cha ujenzi morogoro?
ReplyDelete