Ads

VIJANA KWA KUJITOKEZA KUSHIKA HATAMU KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019

Image result for picha za za bendera ya ccm

Na.Mwanaidi Awadh Kipingu .

Afisa UVccm HQ


Mwamba wa habari
Hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake alikuwa anahimiza sana vijana kujitokeza katika kushiriki masuala mbalimbali ya kujenga taifa kwa manufaaa ya wananchi wote .

Sababu aliamini ili taifa liwe imara na lenye nguvu basi kunahitajika ushiriki mkubwa wa vijana katika maeneo mbalimbali hasa kwenye masuala ya uongozi kuanzia ngazi za chini kabisa .

Mwaka huu wa 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa vijana wengi nchini walijitokeza kwenye kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye serikali za mitaa na vijiji sehemu mbalimbali nchini .

Kwa hakika niwapongeze vijana wote waliojitokeza kwenye kushiriki kwenye harakati za kushika uongozi kuanzia kwenye ngazi za chini kabisa kwa hakika hii inaonyesha ni kwa namna gani vijana wameamka na wameamua kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko katika taifa kuanzia ngazi za chini kabisa katika taifa letu .

Sababu kwa muda mrefu kulikuwa na kasumba nafasi za serikali za mitaa ni kwa ajili ya wazee tu na sio kwa ajili ya vijana bila kujali kuwa maendeleo yeyote huanzia ngazi za chini na huko ndipo panapohitajika kuwa msingi imara kabisa .

Kwa vijana wengi kujitokeza katika nafasi za uongozi katika serikali ya mtaa inaonyesha dira kubwa sana kuwa kundi la vijana sasa limeamka na limeamua kuungana na serikali kwenye kuleta maendeleo kuanzia ngazi za mtaa kabisa lakini pia vijana hao wataleta mabadiliko makubwa kabisa ya kiongozi sababu wananafasi kubwa ya kuendana hasa kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya jemedali Dr. John Joseph Pombe Magufuli yenye nia ya kufanya taifa la Tanzania kuwa na uchumi wa kati na wa viwanda hivyo vijana kwa hakika watasaidiana na serikali katika kufanikisha suala hilo .

Kwa hakika hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere atakuwa anatabasamu kwa kuona vijana wa taifa lake wameamua kushika hatamu kuanzia ngazi ya chini kabisa za mitaa yetu .

Hivyo basi vijana wote waliopata nafasi ya kushika hatamu kwenye nafasi za uongozi kwenye mitaa basi ni wakati wa kuchapa kazi kweli kweli tena kizalendo kabisa ili kuudhihirishia umma kuwa vijana wanaweza kushika nafasi za uongozi .

Ninamatunaini makubwa sana kuwa hata katika uchaguzi wa 2020 vijana wengi watajitokeza kushika hatamu katika uchaguzi mkuu huo ili kuweza kulisukuma gurudumu la maendeleo ya taifa la Tanzania .

Kwa hakika vijana wameamua kuleta mabadiliko ya kiuongozi kuanzia ngazi ya chini kabisa kwa hakika taifa la Tanzania litaanza kujivunia na kushuhudia mabadiliko chanya ya kiuongozi katika nafasi zilizoshikwa na vijana katika serikali za mitaa .




No comments