Ads

TRA Wabuni Mbinu Mpya kukusanya Mapato.

Afisa Mkuu Uhusiano TRA Bi. Oliver Njunmwa (kushoto) akitoa elimu ya ulipaji kodi kwa Mkazi wa Majohe kwa Ngozoma jijini Dar es Salaam.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  imeendelea na kampeni ya kuhamasisha wananchi kulipa kodi ya majengo kwa wakati ili kuhakikisha wanaepukana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

Desemba 11 mwaka huu TRA wakiwa katika mitaa mbalimbali katika mikoa ya kikodi Ilala, Temeke, Kinondoni wameendelea kampeni kwa kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ulipaji kodi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika zoezi la utoaji wa elimu Mkoa wa kikodi Ilala,  Afisa Mkuu Uhusiano TRA Bi. Oliver Njunmwa, amesema kuwa wanaendelea na kampeni ya kuwahamasisha wananchi kulipa kodi ya majengo.

Amesema kuwa watanzania wanapaswa kuwa na utamaduni wa tulipa kodi ikiwemo kodi za majengo jambo ambalo ni rafiki kwa maendeleo ya Taifa.

Bi. Njunmwa amesema kuwa maafisa wa TRA wanatembea mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba kwa ajili kuhamasisha ulipaji wa kodi ya majengo.

"Baada ya kuhamasisha majumbani tunaona wengi wanajitokeza kuja hapa Majohe kwa Ngozoma kuchukua bili kwa ajili ya kwenda kulipa" amesema Bi. Njunmwa.

Amefafanua kuwa kampeni hiyo ni endelevu kwani watakuwa wanafanya kila mwaka, kwani walianza mkoa wa Morogoro, Pwani na sasa wapo jijini Dar es Salaam ambapo wataifanya kazi hiyo  kwa muda wa wiki mbili.

Hata hivyo wakazi na mkoa wa kikodi Ilala wameonekana kufurai huduma za TRA hasa kuwatembelea nyumba hadi nyumba kwa ajili ya kuwakumbusha kulipa kodi ya majengo.

Bw. Ally Juma Mkazi Majohe kwa Ngozoma jijini Dar es Salaam amesema kuwa kampeni hiyo inapaswa kuendelea kwa kila mwaka jambo ambalo litakuwa na faida kwa wananchi kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.

"Serikali inatakiwa kutukumbusha juu ya kulipa kodi, wengi tumekuwa tukisahau kutekeleza wajibu wetu kutokana na sababu mbalimbali" amesema Bw. Juma.

No comments