Ads

KAMPUNI YA INTERSTATE FARM ILIVYO DAHAMIRIA KUWA SAIDIA WAKULIMA WA KAHAWA




Na John Luhende
Mwamba wa habari
Wito umetolewa kwa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania TANTRADE kuongeza matangazo katika vyombo vya habari ilikutoa taarifa zaidi kwa watanzania kujitokeza katika maonesho ya biashara ambayo yamekuwa yakiandaliwa na taaisis hiyo jijini Dar es salaam.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa kampuni ya Inter state Farm (LTD) Bw .Ediger Mapunda alipokuwa akizungumza na mwamba wahabari katika maonesho ya 4 ya bidhaa za viwanda vya Tanzania katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ,barabara ya Kilwa jjini Dar es salaam ambapo alisema kuna haja ya kuongewa nguvu katika utoaji taarifa ili kutoa nafasi zaidi kwa wananchi shiriki maonesho hayo na kujipatia bidhaa zinazo zalishwa nchini .

"Sisi tunapokuja kwenye maonesho tunataka tufikishe ujumbe kwa watu wengi zaidi kwahiyo maonesho yanayo kuja wajitahidi kutangaza zaidi na waongeze hamasa ili washiriki wawe wengi zaidi "Alisema.

Aidha aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kibiashara ikiwemo kupunguza kodi kwewenye mashine upatikanaji wa vibali mbalimbali mfano vibali vya Export sasa unaweza kupata kwa siku moja tofauti na zamani.

Alisema kampuni hiyo imejitahidi kuwaunganisha wakulima wa kahawa Mbinga na kuwafundisha na kuwaelezea ni namna gani ya kuendesha kilimo biashara.

"Tunafanya biashara kwa tofauti na wengine ili kumuwezesha mkulima kufaidika na kilimo katika bidhaa zetu huwa tunaweka alama (QR CODE ambayo inaweza kuscan katika mtandao na kumwekeza mteja katika mashamba ya wakulima abako kahawa hiyo imetoka hii ina msaidia mkulima kupata masoko zaidi ya mazao yake "Alisema

Pamoja na hayo alisema kampuni hiyo imeshiriki maonesho hayo ilikutoa uelewa kwa watanzania kuwa wanaweza kutumia kahawa ya nyumbani ambapo kwa sasa tanzania inauza nje malighafi ya kahawa hivyo waweze kujitokeza kuwekeza ili kahawa isiwe inauzwa kama malighafi iuzwe ikiwa tayari kwa matumizi.

No comments