BINTI MBICHI AELEZA ALIVYOPATA WAZO LA KUANZISHA KIWANDA AKIWA KAZINI.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Msicha aliye kuwa ameajiriwa ameeleza namna alivyo vutiwa na ujasiliamali hatimaye kupata wazo nakuanzisha kiwanda chake mwenyewe akiwa kazini .
Akizungumza na mwamba wahabari Msichana huyo anaye fahamika kwa jina la Shanice James Malugu ambaye nimkurugenzi wa kampuni ya SCRUMMY FOOD PRODUCTS LTD ,alishukuru taasisi alivyo kuwa akiifanyia kazi kwani ndiyo iliyo msaidia kupita mazingira mbalimbali kukutana na wajasiliamali walio mvutia na kuamua kwenda kusomea masomo ya usindikaji mazao (Food Procecing) na kufanikiwa kuanza kutengeneza bidhaa.
''Sikujua chochote kuhusu ujasilia mali siku moja nikiwa katika majukumu ya kazi tulienda SIDO pale nilikuta wanatengeza vitu vingi ikiwemo Pinut bater , Jam, na Pilipili kuanzia hapo nilivutiwa sana nikaona nami namni nitaweza , lakini mimi sikuanza kichwa kichwa baada ya kumaliza masomo (Corse) nikiwa bado niko kazini nilianza kutengeneza nawapelekea kazini wanaona wananiashauri niongeze nini nipunguze nini mpaka nilipo weza nikanunua mashine na kuanzisha kiwanda changu"Alisema
Aidha alisema kutokana na mafanikio aliyo yapata katika ujasiliamali aliamua kulima mazao yake mwenyewe ambayo ndiyo yana msaidia kuendesha kiwanda hicho.
''Ninalima ekali 140 na katika hizi ekali 50 nina lima karanga na ekali 30 nalima Straubell na zingine 60 nalima Nanasi, kilicho nifanya nilime mazao yangu mwenyewe ni kufanya kazi yangu kwa uhakika na kuaminika kwa bidhaa zangu kwani natengeneza ziwe ogarnic yaani zisizo na kemikali huku siweki mbolea yoyote "Alisema .
Alisema watanzania wanaouwezo mkubwa wa kutengeza biadhaa zao wenyewe bila kutegemea vya kutegemea kutoka nje ,naomba watanzania waziamini bidhaa zetu itasaidia kujenga uchumi wa nchi na kuongeza ajira , mfano mimi kwa sasa nimeajiri watanznia watano katika shuguli zangu za kiwanda na kadri nivyo kua nitaajiri zaidi.
Pamoja na hayo aliishukuru Serikali kupita Mamlaka ya maendeleo ya biashara (TANTRADE) kwa kuwapatia fursa wajasiliamali kuweza kujitangaza kwa watanzania kupitia maonesho ya bidhaa za viwanda vya ndani.
Post a Comment