Ads

MAABARA YA TMDA YA KWANZA BARANI AFRIKA KWA UBORA ,INAVIWANGO SAWA NA NCHI ZA BARA LA ULAYA,NCHI ZA AFRIKA ZAPIGANA VIKUMBO KUJA KUJIFUNZA




Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza akitoa maelezo kwa  wananchi walifika katika banda hilo.

Na John Luhende


Mwamba wa habari


Mamlaka ya Dawa na vifaatiba TMDA imesema imefanikiwa kutoa mchango mkubwa wa kitaalamu katika kufanikisha kuajengwa kwa viwanda 12 vya dawa na vifaa tiba jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa Dawa nchini na nje ilikukuza uchumi wa nchi.


Hayo yamebainishwa na Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza ,alipokuwa katika maonesho ya 4 ya bidhaa za viwanda vya Tanzania ambapo alisema pamoja na kufanikisha hilo pia mamlaka itaendelea kuhakisha viwanda hivyo vinakidhi matakwa ya kisheria na viwango vya kimataifa.


''Tumekuja hapa katika maonesho kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi wajuwe majukumu ya hii taasisi na tuanawaeleza nincha kufanya nawao pia kutumia dawana namna ya kuzitumia kwa matumizi sahihi na kuongeza umakini ikiwemo upatikanaji wa dawa."Alisema .

Alisema ,Udhibiti wa Dawa ni dhana pana inahitaji usajili wa dawa ,uchungunzi wa sampuli za dawa inahitaji mifumo mathubuti ,Mamla hii ina maabara ya uchunguzi wa kisayansi kabla ya usaji na kuruhusu dawa kuingia katika soko ,pia kunawakaguzi wako mtaani kufuatilia ubora wa dawa ,ikiwa dawa itakuwa haikidhi viwango na usalama tunaiondoa katika soko .


"Tunafahamu kuwa dawa zote ni sumu ,tunafutiulia pia madha kwa watumiawa dawa hatakama dwai imesajiliwa kama itaonesha madhara makubwa kwa watumiaji tunafania uchungiuzi upya na kuiondoa katika matumizi na Tanzania tunayo maabara inayo tambulika kimataifa na iko katika hatua ya tatu kiuthibiti katika ngazi nne zinazo tambulika kimataifa haya ni mafanikio makubwa


Tanzania imekuwa ni nchi ya kwanza katika bara la Afrika katika kufikia hiingazi yatatu (Maturity level three)ya uthibiti sawa na nchi za ujerumani ,na nchi za bara la ulaya na nchi nyingine za Afrika zinapanga foleni kuja kujifunza namnamifumo inavyo fanya kazi na sasa wanapiga hatua kufikia ngazi yanne ambayo ndiyo ngazi ya juu zaidi ya mwisho dunia kwa sasa .

 


No comments