Ads

CUF Yatoa angalizo Tume ya Uchaguzi, Yafanya ziara kutafuta haki.

Na Noel Rukanuga, Dar esp Salaam
Chama cha Wananchi (CUF) kimewataka wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mtaa kuondoa vigezo kwa wanaoshiriki uchaguzi wa serikali za mtaa kuwa na  namba ya simu kitu ambacho kinadaiwa kitawakosesha haki ya kupiga kura kwa baadhi ya ya watanzania ambao hawana namba za simu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa habari CUF Bw. Abdul Kambaya, amesema kuwa sio kila mtanzania anamiliki simu, kwani kuna wengine hawana simu.

Ameeleza kuwa ni vizuri wakaondoa vigezo hivyo ili kutoa fursa kwa kila mtanzania kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mtaa.

"Kuna baadhi ya vijiji hakuna mawasiliano na hawamiliki simu" amesema Kambaya.

Amesema kuwa wamepata taarifa katika tovuti ya Tume ya Taifa ya uchaguzi ili uweze kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura unatakiwa kuwa na namba ya simu.

Bw. Kambaya amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iondoe hitaji la nambari ya simu katika kujiandikisha katika daftari kudumu la kupiga kura.

Katika hatua nyengine ameeleza kuwa Chama cha CUF kuanzia kesho watakuwa na ziara ya kutembea mikoa yote ya Tanzania.

Bw. Kambaya, amefafanua kuwa lengo la ziara hiyo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mtaa kwa kupeleka kauli ya 'Haki sawa na Furaha kwa wote'.

No comments