Ads

RC MAKONDA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MACHINJIO MAPYA YA VINGUNGUTI, ATOA MAAGIZO MATATU MAZITO MANISPAA YA ILALA*.


Mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo September 29 ametembelea na *kukagua* maendeleo ya Ujenzi wa *Machinjio ya kisasa Vingunguti* ikiwa ni mkakati wake wa *kufuatilia bila kusubiri kuletewa taarifa ofisini* ambapo amewapongeza Shirika la Nyumba la Taifa *NHC* kwa kufanya Kazi *Usiku na Mchana* kwa lengo la kuhakikisha *ujenzi huo unakamilika ndani ya Miezi mitatu* kama ilivyo Matarajio ya *Rais Dkt. John Magufuli.*

Katika ziara hiyo *RC Makonda* amemuelekeza *Mstahiki Meya* wa Ilala *Bw. Omary Kumbilamoto* kuja na Mpango wa kuhakikisha miundombinu ya *Reli inaunganishwa kwenye machinjio hayo* ili Treni iweze kutumika *kupokea wanyama na kusafirisha nyama ndani na Nje ya Nchi.*

Aidha *RC Makonda* amemuelekeza Meya huyo kuhakikisha *ujenzi wa Barabara ya Vingunguti* unaanza Mara moja huku akiitaka *Manispaa ya Ilala* kufikiria uwezekano wa *kulipa fidia kwa wakazi wanaozunguka machinjio hiyo* ili kwa *miaka ijayo* machinjio iweze kupanuliwa na kuwa kubwa zaidi.

Pamoja na hayo *RC Makonda* amesema kuwa tayari *mchakato wa kuagiza mashine mbili za kisasa za Kuchinja na kuchakata nyama* umekamilika ambapo Mashine itakuwa na uwezo wa  kuchinja, kusafisha na kuchakata *Wanyama 2,000* kwa siku moja.

Katika hatua nyingine *RC Makonda amefanya ziara ya kustukiza kwenye Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu na kumuagiza Mkandarasi wa ujenzi wa Soko hilo kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika na kukabidhiwa kabla ya mwezi May Mwakani.*

Hatua hiyo imekuja baada ya *RC Makonda kutoridhishwa kasi ya ujenzi wa soko hilo* ambalo limekuwa *likisuasua* mara kwa Mara huku wataalamu wakitoa taarifa za wongo kuwa ujenzi unaenda vizuri.


No comments