Ads

KADA WA CCM METHUSELA GWAJIMA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI.

Juu ni picha ya Marehemu Mzee Stiven Gwajima.

Mwambawahabari
Mwanasheria na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Methusela Gwajima, amefiwa na Baba yake mzazi Mzee Stiven Gwajima (82).

Katika ukurasa wake wa Instagram Gwajima ameandika

"Nasikitika kuwataarifu kuwa Baba yangu mzazi Mzee Stiven Gwajima amefariki dunia jana  usiku tarehe 30/9/2019 jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

" Nimepoteza rafiki na mshauri wangu ambaye nimeishi naye nyumbani kwangu hapa Sala Sala  Dar es Salaam kwa muda wa miaka 8, hakika nimejifunza mengi na nimeiona faida ya kuishi na wazazi" ameandika Gwajima.

Pumzika kwa Amani Baba yetu, tutakukumbuka daima tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi  jina la Bana lihimidiwe. Amina.

Kwa Mijibu wa taarifa iliyotolewa na Gwajima, ambaye  pia ni Mwanasheria kutoka kampuni  uwakili ya THE  NOBBLE   ATTORNEY 'S,  msiba utakuwa nyumbani kwake Sala Sala Jijini Dar es Salaam.

No comments