Zitto Kabwe Hawezi Kuwa Rais wa Nchi Hii....Haiwezekani soma hapo.

Kesi ya kikatiba kuhusu kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na Mamlaka ya Bunge katika kuwaita na kuwahoji watu mbalimbali, leo inatajwa rasmi mahakamani.
Kesi
hiyo ya Kikatiba namba 01/2019 imefunguliwa Mahakama Kuu, Masjala Kuu
na mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe dhidi ya Spika wa Bunge, Job
Ndugai.
Mahakama
hiyo imetoa wito kwa wadau wote (mdai- Zitto na mdaiwa-Spika) ikiwataka
kufika mahakamani leo kesi hiyo itakapotajwa kwa mara ya kwanza.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Firmin Matogolo, Dk Benhajj Masoud na Elinaza Luvanda.
Katika
kesi hiyo, Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo
anaiomba Mahakama Kuu itoe tafsiri ya kinga ya CAG iliyopo kikatiba na
tafsiri ya Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge katika kushtaki
watu wanaosemekana kulidharau Bunge.
Zitto
alifungua kesi hiyo baada ya Spika kupitia kwenye vyombo vya habari na
baadaye kumwandikia barua CAG, Profesa Mussa Assad akimtaka afike mbele
ya kamati ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli aliyoitoa akiwa Marekani
kuwa Bunge ni dhaifu.
Post a Comment