MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO.
MADIWANI wa Manispaa ya Kigamboni wameitaka manispaa ya kigamboni
kubuni vyanzo vipya vya Mapato kutokana na vyanzo ambavyo Manispaa hiyo ilikuwa ikivitegemea kuchukuliwa na serikali kuu ,jambo ambalo
limesababisha baadhi ya miradi kushindwa kutekelezwa.
Madiwani hao wakichangia katika kikao cha baraza la
madiwani wamesema taarifa zao zimekuwa
zikijirudiarudia kila mwaka kutokana
baadhi ya mambo kutotekelezwa hivyo kulazimu kuandikwa upya .
“Kipindi cha mvua kinaanza muda simrefu namvua zinapo nyesha kichangachui mfereji pale hospitali
,Mahakamani maji yanajaa sijajua mpaka
sasa ufumbuzi wake ukoje , na pia pale stand ya Kigamboni kumekuwa na mrundikano wa magari , nini
mbadala wake na taa hazija wekwa, haya yote nimekuwa nikiyaulizia kila kikao
lakini hakuna utekelezaji “Alisema Dotto Msawa . Diwani wa kakata ya Kigamboni.
Kwa upande wake
Mkurugezi wa Manispaa ya Kigamboni
Ludigija Ng’wilabuzu ,amesema kumekuwa na changamoto nyingi ambazo
zimekuwa zikiibuka kama dharua nje ya bajeti
ikiwemo ujenzi wa madarasa na
madawati na kuwataka Madiwani kuwa wavumilivu na kwamba kila changamoto
itatatuliwa kwa wakati wake kutokana na upatikanaji wa fedha.
Kutokana na hali hiyo Madiwani Isaya Mwita, wa kata ya vijibweni na Sanya
Bunaya, wa kata ya Kimbiji wakitoa mawazo yao kuhusu uanzishwaji vyanzo vipya
vya mapato wameitaka Manispaa kujenga soko la samaki eneo la fery ,kujenga
machinjio ,kujenga majengo ya kitegauchumi (shopping mal) kuweka vizuizi na
kuanza kutoza watu wanaochimba na kusafirisha mchanga ,kokoto na vifusi.
Hata vyo, Diwani wa kata ya Kisarawe two Issa
Hemedi Zahoro ,amepongeza hatua ya Rais John Pombe Magufuli
, kuchukua baadhi ya vyanzo hivyo na
kufafanua kuwa kunafaida kubwa wanaipata kwani wanajengewa Barabara , masoko ,Hospitali.
“Miradi hii inayotekelezwa na serikali kuu thamani yake
ni kubwa inge achiwa Manispaa yetu isingeweza, hata kama tunge achiwa hiyo vyanzo tunavyo lalamikia, nampongeza sana
Rais,
maana halmashauri hizi zilijisahau sana zilikuwa zinafuja mapato, bora
alivyo chukua tujifunze natusipoangalia na kuwa wabunifu halmashauri zitavunjwa”Alisema Zahoro.

Post a Comment