TPB YATOA MSAADA WA FIMBO NYEUPE KWA CHAMA CHA WASIOONA DSM
Mwambawahabari
Benki
ya TPB, imetoa msaada wa fimbo nyeupe 20 kwa chama cha wasioona tawi la
Dar es Salaam, zenye thamani ya sh milioni 1. Msaada huo ulitolewa jana
na Meneja wa Mawasiano wa Benki ya TPB, Bi. Chichi Banda na kukabidhiwa
Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Seif Jega.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Bi Chichi Banda alisema benki hiyo ilitoa
msaada huo kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika jamii.
‘’Katika
uendeshaji wa benki yetu, huwa tuna utaratibu wa kutenga kiasi cha
faida kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii katika maeneo makuu matatu
ambayo ni afya, elimu na ustawi wa jamii’’.
Hivyo
basi tunawaomba wananchi muendelee kutuunga mkono kwa kutumia huduma
zetu za kibenki kwani tunachokipata kama faida, mara zote tumekuwa
tukirudisha kwenu kupitia misaada tunayotoa’’, alisema Chichi.
‘’Tunaamini
msaada huu, utaenda kupunguza changamoto kwa wale wasioona ambao
walikosa kifaa hiki muhimu katika maisha yao’’, aliongeza Chichi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.
Seif Jega, aliushukuru uongozi wa benki ya TPB kwa msaada huo ambao
utawasaidia katika maadhimisho ya Siku ya fimbo cheupe dunia
utakaofanyika kitaifa mkoani Mwanza siku ya tarehe 25 Oktoba 2018.
Katika
maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajia kuwa Makamu wa Raisi, Mhe. Mama
Samia Suluhu. ‘’Kwa kweli tumefarijika sana, kupokea huu msaada kutoka
benki ya TPB, na tunaahidi tutaufikisha kwa wanachama wale ambao
walikuwa hawajapata bado fimbo hizi’’, alisema Jega.
Post a Comment