SERIKALI IMEZITAKA HALMASHAURI KUWA NA ONE STOP CENTRES KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI NCHINI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugezi Mkuu wa
hospitali ya Tumbi Dkt. Edward Wayi akitoa maelezo ya Kituo cha Mkono kwa Mkono
(one stop centre) kwa waandishi wa habali kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia
mapema leo Tumbi Kibaha Mkoani Pwani.
Na Mwandishi wetu
Pwani
Serikali imezitaka
Halmashauri zote Nchini kuhakikisha
zinakuwa na vituo vya huduma za mkono
kwa mkono (Ones Stop Centre) ili kuunga mkono serikali katika juhudi zake za
kupambana na vitendo vya ukatili hapa Nchini.
Hayo yamesema leo
wilayani kibaha mkoani Pwani Naibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea kituo cha huduma
za mkono kwa mkono kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani iliyoko
Kibaha mkoani humo.
Dkt. Ndugulile amesema
kuwa lengo la vituo hivyo linalenga kupunguza mlolongo wa huduma kwa muhanga wa
ukatili kwani vituo hivyo vinatoa huduma za matibabu, huduma za polisi na
ushahuri wa kisaikolojia kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii kwa wahanga wa
ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha Dkt. Ndugulile
amesema nchi kwa sasa ina vituo vikumi tu hivyo kutaka maeneo Mikoa mingine
kuiga Mkoa wa Pwani kuhunga mkono juhudi hizi kwa kuwa takwimu zilizopo zinaonesha
Tanzania ina ina matukio ya ukatili 41,000 na kati ya matukio hayo 13,000 ni
ukatili dhidi ya watoto akitaja hali hiyo kuwa ni ujambazi mpya zidi ya
binadamu.
Amezitaja juhudi
nyingine za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto
kuwa ni kuwepo kwa madawati ya Jinsia katika vituo vya polisi akitaja idadi ya
vituo hivyo kote Nchini kuwa ni jumla ya madawati 500.
Ameongeza kuwa
Serikali inawajengea uwezomwalimu wa Shule za Msingi na Sekondari ili kuwa na
madawati ya ukatili wa kijinsia kwani vitendo vingi vya ukatili kwa watoto
vinatokea katika eneo la shule.
Dkt. Ndugulile pia
ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili vinavyotokea katika maeneo
yao hasa nyumbana katika familia na amesema Serikali itawachukulia hatua watoa
huduma za fya watakaojihushisha na uitoaji wa taarifa za uongo kuhusu mashauri
ya vitendo vya ukatili.
‘’Baadhi ya wanajamii
hapa nchini wanafurahia vitendo vya ukatili kwani wamekuwa wakimalizana
kifamilia na kusababisha vitendo hivi kuendelea” alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri
Ndugulile ameuagiza Mkoa wa Pwani pamoja na mikoa mingine Nchini kuanzisha
dawati la ulinzi wa wanawake na watoto akiongeza kuwa ili ni agizo la serikali
hivyo ni lazima mikoa yote Nchini inakuwa na madawati haya ili kutekeleza agizo
la serikali.
Akiongea na watumishi
wa hospitali ya Tumbi Dkt. Ndugulile amesema kumekuwepo na kasumba ya adaktari ya kuficha ushahidi
kwa watu waliofanyiwa vitendo vya ukatili na kuongeza kuwa hilo ni kosa
kisheria na atakayebainika kuficha ushaidi adhabu yake ni kufutiwa usajili.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile yupo katika
ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Pwani anmbapo anatembelea na kukagua
huduma za afya na maendeleo ya jamii
Post a Comment