Ads

TAIFA STARS KIBARUANI DHIDI YA CAPE VERDE

Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema wako tayari kwa mechi  dhidi ya Cape Verde ambayo itapigwa katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam.

Amunike amesema wameyafanyia kazi makosa yao yaliyotokea katika mechi ya kwanza na kusababisha kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao 3-0.

“Tumepata muda wa kuyafanyia kazi makosa yetu, tunaamini leo hakuna mjadala zaidi ya pointi tatu. Haitakuwa kazi nyepesi lakini tutapambana,” alisema.

Pamoja na marekebisho yaliyofanyika ikiwemo kumuongeza kiungo Erasto Nyoni kutoka Simba, Amunike amesema vijana wake wako katika morali ya juu kabisa.

Mechi hiyo itapigwa saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments